MAKALA YETU LEO




Na Saimeni Mgalula

 APRM ni kifupi cha maneno ya kiingereza "African peer review
mechanism" yaani mpango wa Afrika kujithamini kiutawala bora
,uliobuniwa na Viongozi wa umoja Afrika mwanzoni mwa miaka 2000 ili
kuziwezesha nchi ,wanachama kujithamini kwa kuangaikia namna ya kila
nchi inavyotekeleza kwa usahihi na ufasaha vigezo vya utawala bora na
kubaini changamoto zilizopo ili ziwekewe mkakati wa kugeuza kuwa frsa
za maendeleo.

Kimsingi kuanzishwa APRM ilikuwa ni sehemu ya kutekeleza malengo ya
uliokuwa mpango mpya ya maendeleo wa kiuchumi Barani Afrika (NEPAD)
ambao uliamini kuwepo kwa maendeleo thabiti ya kiuchumi barani humo
kungetegemeana zaidi na kuwepo kwa utawala bora katika siasa ,uchumi
na na huduma muhimu kwa jamii ,NEPAD ilipo asisiwa mwaka 2001 katika
kikao cha nchi za uliokuwa Umoja wa Nchi Huru (OAU) ambao kwa sasa
unaitwa UNO ,ilijiwekea malengo mengi katika kuona uchumi wa Afrika
kwa kiasi na kubaki imara.

Katika utekelezaji wa NEPAD baadaye wataalamu waliona kwamba
kunakuingiliana sana kati ya kukua kwa uchumi na utawala bora katika
siasa "Demokrasia,jamii na uendeshaji wa makampuni.

Ndio maana waliokuwa wajijumuisha malengo ya OAU kwa kanzisha Umoja wa
Afrika (AU) katika mkutano wa mwaka 2002 wakuu wa AU waliona haya ya
kutoa tamko rasmi la kusisitiza nchi za Afrika kuheshimu Demokrasia
siasa safi na utawala bora.

Katika tamko hilo NEPAD iliona kwamba utawala bora ndicho kiini cha
maendeleo yoyote ambayo Afrika ilikuwa ikiyapanga na zaidi tamko
liliweka bayana baadhi ya ya msingi kuangaliwa katika kuona Afrika
inaimarisha utawala bora katika siasa na domokrasia bali pia kiuchumi
na katika huduma za kijamii.

Misingi hiyo ambayo NEPAD iliona ni ya muhimu katika dhana nzima ya
utawala bora ni ni pamoja na kuheshimu haki za binadamu ,uchaguzi
kufanyika kwa mujibu wa sheria,mapambano dhidi ya Rushwa na ufisadi
kuimarishwa,uwazi katika sekta za fedha na mchakato wa bejeti.

Vile vile kuimarisha uwazi,uhuru katika masuala ya ukaguzi wa mahesabu
na mfumo imara wa mabenki ,kuimarisha utawala bora katika uendeshaji
wa makampuni ,kuheshimu ,kulinda na kuenzi hali ya amani na
utulivu,kuhakikisha mipango bora inawekwa kumwendeleza binadamu na
miundo mbinu yake kuwa katika hali bora na mwishoewe kulinda na
kuhimiza usawa wa kijinsia.


Misingi hii ilianzishwa ilikuwa ya muhimu kwa Afrika lakini swali kuu
lilikuwa ni nani angesimamia utekelezaji wake hasa kwa kutambua kuwa
NEPAD ilikuwa na malengo yake mahususi ya kusimamia na kuratibu
utekelezaji wa vigezo vya utawala bora  wa kuangalia pamoja na maswala
mengine ,vipengele vilivyo tajwa hapo juu na namna ya kila nchi
itakayokuwa tayari kwa hiari yake ., ,ijithamini na kuweka mpango
mkakati wa kutatua changamoto zitakazoonekana.

Taasisi hiyo ndio APRM ,ambayo ilikuja kuzinduliwa rasmi katika kikao
cha wakuu wan chi za Afrika katika mkutano wao wa mwaka 2003 baada ya
mkataba wake awali (MOU) kuridhiwa .

Kama ilivyokusudiwa hapo awali wakuu wanchi za Afrika waliona haja ya
kuimarisha Nyanja  ya utawala bora ,hivyo mpango huu unalengo kupitia
mchakato wake tutakao uona punde ,kuhimiza utumiaji wa sera ,viwango
na mienendo inayokubalika kitaalamu Afrika na duniani ili kujenga
utengamano wa kisiasa .

Katika ukuaji wa chanya ya uchumi ,maendeleo endelevu kuharakisha
ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda na hatimaye bara zima pia
kubadilisha uzoefu na kuimarisha mafanikio yaliyofikiliwa sasa.

Matokeo tathimini kuzipa nchi husika nafasi ya kushirikiana kwa kila
moja kujifunza mazuri ya mwenzake ,changamoto nazo kubainisha mbnu
bora za kiutawala kuhimizwa na kasoro kutatuliwa kwa mikakati ya nchi
yenywewe au kwa ushirikiano wa pamoja .

Malengo hayo yanaweza kufkia kupitia mchakato wa APRM unaolenga
kutumia wataalamu wa ndani kutathimini mianya iliopo katika kutekeleza
utawala bora na kutafuta njia za kukabidhiana na udhaifu uliopo .

Kwa malengo haya yanaendelea kubaki mathubutu hata sasa baada ya NEPAD
kubadilisha muundo wake kwa kuunda taasisi ya kuratibu shughuli zake
iliyounganishwa moja kwa moja ndani ya idara za ndani za AU yaani
Nepad planning and coordinating Agency(NPCA)

Katika kutathimini utawala bora mchakato wa APRM unaangalia zaidi
pamoja na viashiria vingine maeneo haya makuu manne ,yaani Demokrasia
na Utawala wa kisiasa ,usimamizi wa uchumi ,utendaji wa mashirika ya
biashara ,maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kwa upendo wa Tanzania ilisaini mkataba wa awali wa makubaliano (MOU)
kujiunga na mchakato wa APRM Mei 26  2004 na kuridhiwa rasmi julai 8
mwaka huo kuwa mwanachama kamili wa mchakato huo.

Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania likaidhinisha mchakato huo
hapo nchini katika kikao chake cha February  mosi 2005 ambapo wabunge
wote waliochangia mjadala huo waliunga mkono hoja na kusisitiza
mchakato huo uanze haraka ili kuiwezesha Tanzania kufaidika na manufaa
ya mpango huo.

Awali ilivyokuwa wizara ya mipango iliteuliwa kuwa wizara unganishi
.hata hivyo baadaye jukumu hilo lilihamishwa kwenda wizara ya mambo ya
nje na ushirikiano wa kimataifa kuwa wizara unganishi kati ya
serikali, APRM Tanzania na makao makuu ya APRM yalioko Afrika kusini.

Hatimaye baraza la Usimamizi la Taifa lenye wajumbe 20 wakiwakilisha
sekta mbalimbali za umma na binafsi kama za dini ,vya siasa asasi za
kijamii na vyombo vya Habari liliunda mwaka 2006 na sekrataeti kuka
iliundwa 2007 na shughuli rasmi za mchakato wa APRM zilianza mwaka
2007.

Sababu za Tanzania kujiunga na mchakato huo ni nyingi lakini akidokeza
nia iliyokuwa nyuma ya uamuzi huo ,Rais Jakaya Kikwete alibainisha
alipokuwa akizindua rasmi Baraza rasmi la Taifa la Usimamizi la APRM
Tanzania kwenye viwanja vya Karimjee Hall ,septemba 11,2009 Dar es
salaam akisisitiza kuwa uamuzi huo ni kwanza kuonesha Tanzania
ikomtayari kuenzi vijenzi vya utawala bora lakini pia ni kutaka
kunufaika na mradi huo.

Hata Elimu kwa umma na uamasishaji kama ulivyo  ona APRM ni mchakato
unao husisha sauti za wadau wenyewe kuanzia wananchi wa kawaida katika
haya wataalamu wa fani anuani wote wakihusishwa na kushirikishwa
katika kutambua na kubainisha maswala ya kiutawala bora.

Hapa nchini mchakato huu chini ya APRM Tanzania ulianza kwa kufanya
uamasishaji kwa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja kwa kufanya mikutano
ya hadha nchi nzima katika kila Mkoa ilichukuliwa sampuli vijiji vine
.

Wizara unganishi ya mambo ya nje ilipewa jukumu lake ilianza mara moja
kwa kutoa taarifa kwea umma kuhusu shughuli za APRM ,ikasimamia semina
nne zilizohusisha wadau mbalimbali.

Semina hizo ndizo zilizosaidia kupata wawakilishi wa kuunda Baraza la
Taifa la Usimamizi ambalo kwa zaidi kidogo ya asilimia 80 linawajumbe
kutoka sekta binafsi ilikufanya mchakato kuwa huru kutoka mikono ya
serikali .

Pia APRM Tanzania ilipata kuchapisha kijarida kilichokuwa na kurasa
nane ambachokilichapishwa katika miezi ya April na Julai 2008 na
nakala zipatazo 90,000 zilichapishwa na kusambazwa kwa umma kwa njia
ya kuingizwa katika moja ya magazeti makuu yanayochapishwa kila siku
na kuwafikia watu wengi .

Hata hivyo nyaraka zenye taarifa mbalimbali kuhusu APRM zipatazo 6,660
zilisambazwa kwa wadau hata hivyo kijarida hicho kiliwekwa kwenye
tovuti ya APRM yaani 
WWW.aprmtanzania.org, kwa taarifa nyingi zaidi .

Katika mkakati mpya wa mawasiliano kwa umma wa miaka mitano ijayo njia
za kisasa za mawasiliano pia zimedhinishwa kutumia na tayari wadau wa
APRM wanaweza kupata taarifa zaidi.

MWISHO.
Previous
Next Post »