Naibu waziri kilimo na Chakula Adam Malima, akizungumza baada ya kuzindua maadhimisho ya siku ya kutafuna korosho yaliyofanyika katika maonyesho ya biashara Sabasaba jijini Dar es Salaam. |
Mteja akinunua Korosho katika banda la maonyesho ya Saabasaba Dar es Saalaam wakati wa kilele cha siku ya kuonja korosho nchini Julai 05 mwaka huu.
Mfanyakazi wa bodi ya korosho , Juma Kimante akigawa korosho kuadhimisha siku ya kuonja korosho.
WATANZANIA wameaswa kujenga utamaduni wa kupenda kula korosho kwani zinajenga afya hususani kwa akinamama wajawazito na watoto wadogo, ambao huwezeshwa katika makuzi bora.
Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Kilimo na Chakula, Malima wakati akizindua siku ya kuonja korosho kwenye banda la bodi ya korosho lililopo kwenye maonyesho ya sabasaba.
Waziri Malima alisema kuwa Tanzania inasifika du niani kwa kulima korosho safi na bora lakini wananchi wake hawana utamaduni wa kula hizo kororosho badala yake wanapendelea kula biskuti jambo ambalo ni kinyume na nchi zingine.
“Watanzania hatupendi kulakorosho wakati zinapatikana kwa wingi hapa nchini ,nawaasa wazazi wajitahidi kila wanapoandaa chakula korosho iwe pembeni kwa sababu ni nzuri hata kwa watoto…..pia naiagiza bodi ya korosho kutengeneza vipindi vya kuhamasisha ulaji wa korosho vichezwe kwenye redio na televisheni”amesema Waziri Maalima.
Naye Katibu Mtendaji katika mfuko wa kuendeleza korosho nchini (CIDTF) Suleman Lenga amewashauri wakulima kutambua kuwa hapa nchini kuna soko kubwa la korosho badala ya kutegemea soko la nje wanaweza kuuza hapa.
“kwa kutambua hilo mfuko wa CIDTF umeambua kuwalipia gharama za kubangua korosho wakulima wadogo ili waweze kuziongeza thamani wakati wa kuuza hivyo wananchi wanapaswa kuanza kulakorosho kwa wingi ziweze kuletwa sokoni kwa wingi pia”amesema Lenga.
EmoticonEmoticon