Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
amewapiga marufuku waganga wakuu wa hospitali na vituo vya afya vya umma
nchini kuwatoza gharama za vipimo na matibabu watoto wanaofanyiwa
ukatili wa kijinsia ikiwemo vitendo vya ubakaji.
Dk. Ummy ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
“Nafuta
tozo ya kumuona daktari na matibabu kwa watoto wanaobakwa ili
kuwasaidia wasio na uwezo kupata matibabu na kufanyiwa vipimo
vitakavyowezesha upatikanaji wa ushahidi ili wahusika wachukuliwe hatua
za kisheria, ” amesema.
Ameongeza
kuwa “Narudia tena fedha ya kumuona daktari marufuku, sitakuwa na
msamaha kwa mganga mkuu ambaye hospitali yake itawatoza fedha Mama
mjamzito, mtoto wa chini ya miaka mitano na wazee.Muhimbili niiagize
kuwa hakuna fedha za kumuona daktari na vipimo, lakini kwenye dawa
nitaelewa kwa kuwa wanawajibu wa kuchangia, wananchi wanakatwa kodi
ambazo hulipa madaktari mishahara na kununulia vifaa tiba. “
Dk.
Ummy amesema anataka kuboresha usimamizi wa huduma za afya kwa waganga
wakuu wa mikoa ili kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za afya.
“Bila ya kusimamia utekelezaji na uwajibikaji katika sekta ya afya huduma ya afya haitakuwa nzuri, ” amesema.
EmoticonEmoticon