Rais
wa uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa shambulizi la bomu la
kujitoa muhanga lililofanywa siku ya Jumamosi katika mji wa Gaziantep
lilifanywa na mtu anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 12 na 14.
Erdogan
amesema anaamini kuwa wapiganaji wa kundi la Islamic State huenda
wakawa wametekeleza shambulizi hilo, ambalo limeuwa zaidi ya watu 50
waliokuwa kwenye harusi ya kikudishi.
Hili
linatajwa kuwa ni shambulizi kubwa zaidi kutokea kwa mwaka huu nchini
humo huku wapiganaji wa IS wamepoteza ardhi katika Jirani na Kaskazini
mwa Syria.
Ripoti
zinasema kuwa waasi wanaoisaidia Uturuki wanajiandaa kukabiliana nao
katika mipaka kati ya nchi hizo mbili, huku Naibu Waziri Mkuu Mehmet
Simsek amesema mlipuko huo ni kitendo cha kinyama huku akiongeza kuwa
huenda lilitekelezwa na wapiganaji wa kujitoa muhanga.
Rais
Erdogan ameongeza kuwa hakuna tofauti kati ya IS, Vuguvugu lililopigwa
marufuku la PKK na wafuasi wa kiongozi wa kidini aliyeko uhamishoni
nchini Marekani Fetullah Gulen ambaye alilaumiwa kwa kupanga jaribio la
mapinduzi lililotibuka mwezi uliopita.
EmoticonEmoticon