TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 27.01.2015.
·
MTU MMOJA MKAZI WA KITONGOJI CHA CHANG’OMBE
AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI.
·
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MKUTANO WILAYANI
MOMBA AUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA SHAMBANI.
·
MTU MMOJA MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA AFARIKI
DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA SEMI TRALLER.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWINZALA SEKELE MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 40 – 45 MKAZI WA KITONGOJI CHA
CHANG’OMBE – MSHEWE ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA
KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UMETELEKEZWA MNAMO TAREHE 26.01.2015 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI NA
KATA YA MSHEWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA
MBEYA.
INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI KULIPIZA KISASI
KUFUATIA MAREHEMU KUTUHUMIWA KUHUSIKA KATIKA TUKIO LA MAUAJI YA SEKELA KAINI MKAZI WA KIJIJI CHA MSHEWE
AMBAYE ALIKUTWA AMEUAWA NA KUTUPWA KATIKA SHAMBA LA MAHINDI KIJIJINI HAPO
TAREHE 24.01.2015 MAJIRA YA SAA 15:45 ALASIRI.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WALIOHUSIKA
KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA
WAKATI UCHUNGUZI NA UPELELEZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MKUTANO WILAYNI MOMBA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HAMIS SIMWAWA
(25) ALIKUTWA AMEUAWA SHAMBANI KWA KUKATWA SHOKA SHINGONI NA KISHA
KUNYOFOLEWA VIUNGO VYA MWILI AMBAVYO NI ULIMI, MENO YA CHINI NA JICHO LA
KUSHOTO.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA SHAMBANI MNAMO TAREHE 26.01.2015 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI
CHA MKUTANO, KATA YA NZOKA, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA KABLA YA WATU HAO KUFANYA TUKIO HILO WALIMWITA MAREHEMU ILI
AWASAIDIE KAZI ZA SHAMBANI NA KISHA KUMUUA.
INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI IMANI ZA
KISHIRIKINA. WATUHUMIWA WAWILI WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. KAWAWA SINKALA (31) NA 2. EMANUEL SINKALA (15) WOTE WAKAZI WA
KIJIJI CHA MKUTANO.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA JOSHUA ANDENDEKISYE
MWAISANILA (35) ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA
USAJILI T.189 BLK/T.193 BLK AINA YA
SEMI TRALLER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE AHAZI CHEYO (24) MKAZI WA IYUNGA JIJINI MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.01.2015 MAJIRA YA SAA
09:05 ASUBUHI HUKO FOREST KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA
AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI
PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOEPUKIKA.
Imeasainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
EmoticonEmoticon