Vitamin D ni vitamini muhimu ambayo husaidia mwili kufanya kazi. Upungufu wa vitamini hii unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya kuanzia udhaifu wa mifupa,matatizo ya nywele na hata udhaifu wa misuli. Jua huchukuliwa kama chanzo bora cha vitamini D; lakini hata hivyo si vyema kukaa juani muda mrefu. Kwa hiyo ili kuongeza kiwango cha vitamini D katika mwili ngazi, hivi ni baadhi vya vyakula ambavyo vina kiasi kikubwa cha vitamini D.
Uyoga unaweza kuzalisha vitamini D wakati unapokuwa juani. Uyoga ni moja ya vyanzo vyenye vitamini D kwa kiasi kikubwa.Pia hutoa vitamini B5 na madini ya shaba.
Mafuta samaki
Samaki wenye mafuta kama salmon, trout, tuna, sangara nk wana kiwango kikubwa cha vitamini D. Pia wana kiasi kikubwa cha mafuta ya omega 3(omega-3 fatty, ambayo yanafaa kwa afya ya moyo wako.
Cod liver oil
Cod liver oil ni maarufu kwa kuongeza vitamini D. Ina kiwango cha juu cha vitamini D na vitamini A.
Kiini cha yai
Kiini cha yai kina kiasi kikubwa cha vitamini D. Mbali na hilo pia , ni chanzo kizuri cha protini na vitamini B12.
Vyakula vilivyoongezwa vit D
(Fortified products)
Vitamin D pia inaweza kupatikana kutoka katika vyakula ambavyo vimeongezewa vitamini hii. Bidhaa nyingi kama maziwa ya ng'ombe, soya, maji ya machungwa, nafaka nk zinaweza kuongezewa vitamini D. Soma vibandiko vya vyakula ili uweze kubaini ni vipi vina kiasi kikubwa cha vitamini D.
EmoticonEmoticon