Watoto
wenye Albinism, wakipata "msosi", wakati wa hafla ya chakula cha mchana
kila mwaka inayoandaliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald
Mengi, kwa watu wenye ulemavu. Hafla ya mwaka huu ilifanyika pale ukumbi
wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, siku ya Jumapili Januari 25,
2015. Kwa uchache watu 4,000 walihudhuria hafla hiyo.
MWENYEKITI
Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, Jumapili Januari 26, 2015, kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, aliwaalika watu wenye
ulemavu kiasi cha 4,000 kwenye hafla ya kila mwaka ya chakula cha
mchana.
Dkt. Mengi alishiki kula nao chakula cha mchana ikiwa ni pamoja na kuwahudumia kwa kuwagawia vyakula baadhi yao.
Kama
ilivyo ada, wageni wake hao walikula, walikunywa na kucheza muziki,
ambapo wasanii mbalimbali mashuhuri hapa nchini wa muziki wa kizazi
kipya yaani BONGO Flava, walitumbuiza.
Jambo
jipya lililojitokeza kwenye hafla ya mwka huu, Dkt. Mengi aliwatangazia
“Bingo” watu wenye ulemavu kote nchini, kuwa ataanzisha shindano la wazo
bora la shughulki ya kibiashara itakayomkomboa mtu mwenye ulemavu,
ambapo atatenga shilingi milioni 10 kila mwezi kwa washindi kumi
kujinyakulia shilingi milioni 1 kama mtaji wa kunzia shughuli
iliyopendekezwa kama wazo.
Hali
kadhalika, hafla ya mwaka huu imekuja na neema kwa watu wenye ulemavu wa
viungo, ambapo kampuni ya Kamal Steels imeahidi kutoa miguu bandia 200
kila mwaka kuwasaidia watu wenye ulemavu wa viungo kote nchini, na kwa
kuanzia kwenye hafla hiyo palitolewa miguu hiyo bandia 200.
Picha kwa hisani ya K-VIS Blog
EmoticonEmoticon