· MTU MMOJA AUAWA NA KUNDI LA WANANCHI KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI.




TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 10.06.2014.


·         MTU MMOJA AUAWA NA KUNDI LA WANANCHI KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI.


·         WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI WAKIWA NA MALI ZIDHANIWAZO KUWA ZA WIZI.


KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA PETRO KIBONA (30) MKAZI WA KIJIJI CHA HALUNGU ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA  SERIKALI WILAYA YA  MBOZI BAADA YA  KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA   SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI  WAKITUMIA SILAHA ZA JADI MAWE,FIMBO NA RUNGU.

TUKIO HILO LIMETOKEA MAJIRA YA SAA 03:00 USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA KITONGOJI CHA SHULE- MLOWO, KATA TA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU KUKAMATWA AKIWA ANAIBA PIKIPIKI NYUMBANI KWA ARON BANED (36) AFISA MTENDAJI KATA YA MSIA, MKAZI WA MLOWO MAJIRA YA SAA 01:30 USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA KITONGOJI CHA SHULE, KATA YA MLOWO.

WAKATI WA TUKIO MHANGA ALIJERUHIWA MKONO WA KUSHOTO KWA KUKATWA SHOKA DOGO ALILOKUWA NALO MAREHEMU. PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.994 ARB AINA YA TOYO IPO KITUO CHA POLISI MLOWO. UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.



TAARIFA ZA MSAKO:

WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. BRAUN KAMWELA (30) NA 2. GABRIEL MWAMBENE (30) WOTE WAKAZI WA KIWIRA WAKIWA NA TV AINA YA PANASONIC 2 NA REDIO AINA YA SONY 2 MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI.  

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 09.06.2014 MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU KATIKA ENEO LA KIWIRA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA   UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA.


Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »