- Huzalishwa kwa njia ya chupa
- Mche mmoja huzalisha zaidi ya miche 100
“WATU wanalalamika tu migomba yao
inaharibika, lakini hawajui tatizo hasa ni nini,” anasema mkazi wa Kyela,
Emmanuel Mwandambo.
Kyela ni miongoni mwa maeneo walimayo ndizi japo si kwa kiwango kikubwa mfano kwenye Wilaya ya Rungwe. Kwa wakulima wengi, kilimo cha ndizi ni kile cha mazoea.
Wakulima wa zao hilo la ndizi kwa wilaya hiyo ya Kyela hawana uelewa wowote wa magonjwa yanayosumbua zao hilo na wala uelewa kuhusu kuwepo kwa migomba inayozalishwa ikiwa haina magonjwa.
Wakati wakulima hao wakiendelea na kilimo chao cha mazoea na kisicho na tija cha zao hilo la ndizi, wenzao wa Kijiji cha Hembeti mkoani Morogoro hali ni tofauti.
Wakulima wa Hembeti wameanza kutumia miche iliyozalishwa kwa njia ya chupa ambayo hutumika kuzalisha miche ya migomba isiyokuwa na magonjwa.
Wakulima wa ndizi katika Kijiji hicho cha Hembeti wamebahatika kuwa wanufaikaji wa awali wa aina hiyo ya migomba baada ya Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) mkoani Morogoro kuweka shamba darasa kijijini hapo kwa ajili ya kutoa elimu ya aina hiyo ya migomba kwa wakulima.
Kilichowakomboa wakulima hao wa ndizi katika Kijiji cha Hembeti ni taarifa waliyopatiwa kuhusu uwepo wa teknolojia hiyo, na watafiti kuwapa mafunzo ya njia bora za kilimo cha ndizi, nafasi ambayo wakulima wengi, wakiwemo wale wa wilaya za Kyela na Rungwe, hawajabahatika kuipata.
Kutokana na pengo hili la taarifa kati ya watafiti wa kilimo na wakulima nchini, Mradi wa Tafiti Bunifu za Kilimo (iAGRI) umekuja na suluhisho kwa kuwashirikisha waandishi wa habari katika usambazaji wa taarifa mbalimbali zihusuzo tafiti za kilimo zinazofanyika SUA.
Hivi karibuni, iAGRI iliwakutanisha waandishi wa habari mjini Morogoro kwa mafunzo kuhusu uandishi wa habari za tafiti za kilimo ambapo katika ratiba yao ya mafunzo walitembelea pia SUA kujionea tafiti mbalimbali zinavyofanyika.
Miongoni mwa tafiti hizo ni teknolojia inavyotumika kuzalisha miche ya migomba kwa njia ya chupa ili kupata miche bora isiyokuwa na magonjwa na kwa wingi.
Mkulima mwenye kutumia miche hiyo ya migomba hunufaika kutokana na ubora wa mazao yatokanayo na migomba hiyo, ikiwemo mikungu mikubwa ya ndizi na wakulima hao huweza kuuza miche kutoka kwenye mashamba yao yenye migomba hiyo bora kwa wenzao hivyo kueneza aina bora za migomba kwa wakulima wengi zaidi.
Mtaalamu wa zao hilo la ndizi anainisha aina mbili za ugonjwa wa migomba wenye kusumbua zaidi wakulima nchini, na wanazitaja aina hizo kuwa ni SIGATOKA NYEUSI na MNYAUKO WA MIGOMBA.
Kwa mujibu wa wataalamu hao, ugonjwa wa sigatoka nyeusi huathiri zaidi majani ya migomba, ambapo dalili yake kuu ni majani kubadilika rangi kutoka kijani na kuwa na mabaka meusi. Aina bora za migomba zenye ukinzani wa ugojwa huo zimeweza kuzalishwa kwa wingi.
Hata hivyo kwa wakulima wa zao hilo mkoani Mbeya, rangi hiyo haina maana yoyote kwao, huichukulia kimazoea kuwa ni kawaida majani kubadilika rangi.
Mnyauko wa migomba unatajwa kuwa ugonjwa hatari zaidi, kutokana na tabia yake ya kuathiri mgomba mzima kiasi cha kuua kabisa, na mbaya zaidi, husambaa kwenye migomba mingine kwa haraka zaidi tofauti na sigatoka nyeusi. Aina za migomba yenye ukinzani wa ugojwa huu ziko kwenye hatua za awali za utafiti.
Migomba isiyo na magonjwa inavyozalishwa
Kutokana na kubainika kwa magonjwa haya katika baadhi ya maeneo ya nchi, watafiti katika Chuo Kikuu cha Kilimo, Sokoine walilazimika kutafuta utatuzi wa kitaalamu wa tatizo hilo, na ndipo walipokuja na matumizi ya teknolojia ya chupa (tissue culture) katika kuzalisha miche ya migomba isiyo na maradhi.
Mtafiti wa Mimea na Vipando, Deogracius Protas anaielezea teknolojia ya vipando kuwa yenye manufaa zaidi katika kuokoa mimea iliyo hatarini kupotea, na kutoa mfano wa mmea aina ya “carrisa,” ambao ni mti unaotumika kutengeza mbao. Kwa kutumia teknolojia hiyo wameweza kuuzalisha kwa wingi na kuutunza.
“Mimea mingi duniani ipo hatarini kupotea kutokana na kushambuliwa na magonjwa au kwa kuharibiwa na binadamu. Tunatumia njia hii kuzalisha mimea hiyo kwa kutumia sehemu ya mimea hiyo kuzalisha mimea mingi zaidi na isiyo na maradhi,” anasema Protas.
Teknolojia hii huzalisha kwa mfumo ujulikanao kitaalamu kama “asexual reproduction,” kwa maana kwamba ni mfumo wa kuzalisha pasipo kutumia muunganiko wa mbegu dume na jike.
Mtafiti Protas anasema teknolojia ya hiyo hutumia mfumo unaozalisha miche kwa kutumia tishu katika mchakato unaoanzia maabara.
Hata hivyo mtafiti huyo anafafanua kuwa teknolojia hiyo haijihusishi na tabia za mimea, kwa maana kwamba haishughuliki na ubadilishaji wa chembe hai “genes.”
Hatua ya kwanza, kwa mujibu wa mtafiti huyo, huenda kwenye shamba na kuchagua mgomba ambayo haujambukizwa. Kipande huchukuliwa kutoka sehemu inayohusiana na uotaji wa mgomba kwenye shina.
Kipande hicho huchukuliwa hadi maabara ambako hatua za awali za uzalishaji miche hufanyika.
Maabara ni moja ya mahitaji muhimu katika uzalishaji miche isiyokuwa na magonjwa. Mahitaji mengine ni pamoja na madawa na wataalamu.
Kuna sehemu nne muhimu katika maabara za teknolojia ya uzalishaji wa miche kwa njia ya chupa, ambazo ni pamoja na ile ya matayarisho ya sampuli, chumba kinachotumika kuzihifadhi sampuli zilizowekwa kwenye chupa (test tubes) zikiwa na virutubishi, sehemu ya kuzalishia na sehemu ya kuhifadhi mimea iliyooteshwa.
Protas anaitaja sifa ya usafi katika maabara kuwa ni ya msingi na isipozingatiwa husababisha kupatikana kwa matokeo mabaya. Kutokana na kuzingatia usafi katika kiwango cha juu, watu hawaruhusiwi kuingia na viatu na pia hutakiwa kufunika pua kwa vifaa maalumu.
Katika maelezo yake kwa waandishi wa habari za utafiti wa kilimo, Mtafiti Protas anaelezea mchakato huo hatua kwa hatua akisema.
“Katika hatua ya kwanza, “initiation stage,” kipande kilichochukuliwa kutoka kwenye mgomba huwekwa kwenye chupa (test tube) yenye virutubisho 12 tofauti (micro and macro nutrients) kukuzia, na baadaye hupelekwa kwenye chumba chenye giza.
“Baada ya wiki mbili, tunaangalia maendeleo , kama mazuri, kile kipande kitaanza kuchipua, ndipo kinahamishiwa kwenye chombo kingine. Chupa kubwa zaidi, kwa ajili ya kutoa machipukizi. Hapa mazingira ni rafiki zaidi kwa mmea, kwani unapata mwanga saa 16 na giza saa nane.”
Mtafiti huyo anabainisha kuwa katika hatua hiyo, inayofahamika kama “proliferation or multiplication stage,” hutumia siku 14 kabla ya kuhamia katika chumba kingine katika hatua ya tatu. Katika hatua hii ya pili yawezekana pia kipande kisichipue au kupata maambukizi ya ugonjwa hivyo huachwa na kuchukuliwa vile vilivyo bora tu kwa hatua ya tatu.
Katika hatua ya tatu, au “rooting stage,” kama inavyofahamika kitaalamu, watoto waliooteshwa wanahamishiwa kwenye vyombo vingine, chupa kubwa zaidi kwa siku 14 zingine kwa ajili ya kutoa mizizi.
“tunazingatia usafi katika kiwango cha juu sana kuepuka maambukizi yaani “contamination,” anasema Protas.
Kutoka hatua ya kwanza, pale kinapochukuliwa kipande cha mgomba hadi hatua ya tatu ya kuotesha mizizi, hutumia mwezi mmoja na nusu, kwa maana ya siku 14 kwa kila hatua na kile kipande kilichoteshwa huweza kuzalisha watoto zaidi ya 100.
Protas anasema, baada ya hatua hiyo ya tatu huchambua watoto waliopatikana, ni wale wenye afya nzuri tu na wasio na maambukizi yoyote ndio huhamishiwa kwenye vifuko maalumu vilivyoshindiliwa makumbi ya nazi, yaliyosangwa na kuchemshwa kuzuia maambukizi.
Anasema, machipukizi hayo, yakiwa kwenye hivyo vifuko, huhamishiwa nje na kuwekwa kwenye banda maalumu kwa ajili ya kuendelea kukua na baada ya mwezi mmoja uhamishiwa kwenye vitalu vikubwa kuendelea kukuzwa ili iwe tayari kwa kuuzwa.
“Kuanzia hatua ya kwanza kule maabara hadi kukuzwa huchukua miezi mitano na nusu, na baada ya hapo mgomba huwa tayari kwa kupelekwa shambani kupandwa, unakuwa hauna ugonjwa na utatoa watoto wasio na ugonjwa, mazao yaliyo bora,” anasema Protas.
Nini faida ya utafiti huo;
Utafiti wa kutumia teknolojia ya uzalishaji wa migomba kwa njia ya chupa una faida kubwa, ambazo, kwa mujibu wa mtafiti Protas, ni pamoja na mche mmoja wa mgomba kuzalisha miche zaidi ya 100 isiyo na ugonjwa, ambayo nayo itazalisha machipukizi bora yasiyokuwa na ugonjwa.
Migomba iliyozalishwa kwa kutumia teknolojia hiyo, iwapo itatunzwa vizuri, basi hutoa mazao mengi na bora kuanzia uzao wake wa kwanza.
Hata hivyo, Protas anazitaja changamoto zinazowakbili kuwa ni pamoja na tatizo la fedha za kuendeshea tafiti zao, hivyo kuathiri maendeleo ya tafiti zao.
“Mradi ulianza kwa fedha za wafadhili, lakini hivi sasa hawapo, tunaendesha kwa kutegemea fedha kidogo tunazapata, wakati mwingine tunakwama kuendelea na utafiti kutokana na kukosa fedha,” anasema Protas.
Mtafiti huyo anaitaja changamoto nyingine kuwa ni upatikanaji wa madawa ikizingatiwa kuwa wanategemea kuagiza kutoka nje ya nchi na wakati huo huo kunakuwa na tatizo la fedha.
Watafiti hao hukabiliwa pia na tatizo la kukatika umeme mara kwa mara linaathiri tafiti, hususani wanapokuwa katika hatua ya maabara. Lakini suala la wageni kutembelea maabara hiyo ni tatizo jingine pia kwao, kutokana na hofu ya kuingiza vimelea vya magonjwa.

RAIA MWEMA
Watafiti SUA wazalisha miche ya migomba isiyokuwa na magonjwa
Toleo la 396
11 Mar 2015
- Huzalishwa kwa njia ya chupa
- Mche mmoja huzalisha zaidi ya miche 100
“WATU wanalalamika tu migomba yao inaharibika, lakini hawajui tatizo hasa ni nini,” anasema mkazi wa Kyela, Emmanuel Mwandambo.

Tufuatilie mtandaoni:
fkyembe@gmail.com
+255-713290487
Endelea Kuhabarika
Toa maoni yako

EmoticonEmoticon