Huyu ndiye Mchezaji aliyefariki akiwa uwanjani.


Sylvain-Azougoui

Hii ni taarifa ya kusikitisha ambayo hutokea mara chache kusikia mchezaji amefia wakati mechi ikichezwa au alipata matatizo uwanajan mpaka kupelekea umauti,Mchezaji kutoka  klabu ya Ac Bongoville Sylvain Azougoui amefariki baada ya kupigwa teke ya kichwani wakati wa mechi ya ligi kuu nchini Gabon.

Mchezaji huyo ambaye ndiye alikua Kipa alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya matatizo hayo wakati wa mechi yao dhidi ya klabu ya Centre Mberi Sportif,Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Togo alikuwa amelisimamisha kombora lililopigwa langoni mwake,lakini baadae mshambulizi alipoteza mwelekeo na kumkanyaga Azougoui kichwani.

Mechi hiyo ambayo ilichezwa Jumapili April 20 uwanja wa Bongoville ambao uko umbali wa kilomita 800 kutoka Libreville mji mkuu wa Gabon
Previous
Next Post »