PESA INVYOWATESA MASTAA WA NOLLYWOOD

 


Uche Jumbo
KATI ya vitu ambavyo wanawake wanavithamini na kuvipa kipaumbele katika masuala yao ya urembo, ni nywele na kucha.Kwao ndio kama kitambulisho cha urembo hasa kwa mabinti wa kisasa.

Ndio maana wamekuwa wakitunza nywele na kucha zao kwa gharama yoyote ile na kila siku wamekuwa wakitumia teknolojia za kila namna.

Lakini pesa haina adabu. Kwa Nollywood wapo mabinti ambao wamewekewa fedha mezani wakanyoa nywele zao.

Wameshawishiwa kwa fedha na maprodyuza wakanyoa nywele ili kuendana na uhusika kwenye filamu zilizolengwa. Mbali urembo wengine wamekuwa wakishawishiwa hata kujikondesha. Fuatilia orodha hii;

Mercy Johnson
Mercy Johnson ni miongoni mwa mabinti wanaoangaliwa sana, yaani kwa kifupi ameiteka Nollywood.

Miaka miwili iliyopita alishiriki filamu ya 'Heart Of A Widow' kama mjane na akalazimika kunyoa nywele zake baada ya kukubaliana dau na prodyuza.

Kwa mujibu wa ripoti, Mercy alipewa dau nono kuliko alivyochuma katika filamu zote alizowahi kuigiza. Alivaa uhusika vilivyo na kuonekana kweli ni mjane.

Uche Jombo
Uche Jombo alipoteza uzito kwenye filamu hii ya 'Holding Hope'. Aliifanya na Emem Isong mwaka jana. Alilazimika kujikondesha kwa muda ili kuigiza ni mwanamke mwenye kansa.

Akiwa katika kujikondesha, watu ambao walikuwa hawajui walipakazia kwamba ametoa ujauzito wa miezi sita.

Uvumi huo ukamuathiri kiasi, lakini baadaye wazushi walikuja kuumbuka baada ya ukweli kubainika kwamba alilazimishwa kujikondesha ili aigize filamu.

Baadaye ilimchukua muda kurejea kwenye afya yake ya kawaida.

Nuella Njubigbo
Hata yeye mwaka jana alinyoa nywele ili 'kufiti' kwenye uhusika wa filamu moja ambayo ilishangaza wengi. Hakuna aliyetarajia kwamba binti huyo angeweza kufanya kilichotokea. Baadaye mashabiki wakaishia kusema 'fedha haina adabu'.

Oge Okoye
Mwaka jana aliigiza pia kama mjane. Hali hiyo ilimlazimu kunyoa nywele zake ili aendane na hali halisi ya matatizo anayopata mwanamke mjane aliyekuwa amezoea kuishi maisha mazuri.

Kama ilivyokuwa kwa wenziye; Mercy Johnson na Stella Damasus, naye alionyesha umahiri wake.

Si wengi waliobahatika kuiona filamu hiyo kutokana na usambazaji wake kutokuwa mkubwa, lakini walioitazama wamesifu.

Adaora Ukoh
Kwenye filamu ya 'Thy Kingdom Come' alilazimika kunyoa akavaa uhusika wa mjane aliyerudi kijijini akalazimishwa na tamaduni kubadilika na kuachana na mambo ya kisasa kama kuwa na nywele za kisasa.

Alishirikiana na wenzie kama Sam Dede, Mike Ezuruonye na Kenneth Okokwo.
Previous
Next Post »