Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (Pichani)
amemtumia salamu za rambirambi Kipa wa Young Africans na timu ya
Tanzania ‘Taifa Stars’, Deogratius Munishi kutokana na kifo cha Baba
yake mzazi, Mzee Boniventur Munishi kilichotokea jana Agosti 28, 2016.
Rais
Malinzi amepokea taarifa za kifo cha Mzee Boniventur Munishi mara baada
ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Young Africans na
African Lyon uliofanyika jana Agosti 28, 2016 ambako Deogratius
aliongoza timu yake Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 bila
kufahamu kuwa amepoteza baba.
“Ni
ujasiri wa aina yake aliokuwa nao Kipa Munishi kwenye mchezo wa Ligi
Kuu bila kuonyesha tofauti,” amesema Malinzi ambaye katika zake za
rambirambi kwenda kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki
amewataka kuwa na moyo wa subira wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa
wao.
Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu Mzee Boniventur Munishi mahala pema peponi.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.
EmoticonEmoticon