Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi
akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda Baada ya
kuwasili mkoani humo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akizindua
mpango kabambe mkoani Mtwara na Mkukabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi.
Halima Dendego.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua
mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi katika Halmashauri ya
Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi yanafanyika kwa ukamilifu.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua
masijala ya ardhi halmashauri ya Manispaa ya Mtwara na kuwataka Maafisa
Ardhi kuweka kumbukumbu za Hati Miliki za Ardhi katika mpangilio mzuri
ili kuepusha migogoro ya ardhi..
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiongea
na wananchi wa mkoa wa Mtwara katika uzinduzi wa Mpango Kabambe Mkoani
hapo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (wapili
kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego (wakwanza kushoto),
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda (wakwanza kulia), Mwenyekiti
wa CCM Mtwara Ndugu Muhamed Sinani (wapili kulia) wakiwa katika uznduzi
huo.
Wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakifuatilia Uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya Mtwara.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.
Ndugu Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa ya Mtwara akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi amefanya
uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya 2015-2035 Mkoani Mtwara .
Katika shughuli hiyo Mh. Lukuvi aliwataka watendaji wa Mtwara katika
sekta ya ardhi kwa kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa Bi. Halima
Dendego kuhakikisha kuwa wanafuata Master Plan hiyo ili kuweza kuipanga
Mtwara na kanda ya kusini yote vizuri hatimaye kufikia Tanzania yenye
uchumi wa kati na Viwanda.
Katika
ziara hiyo, mbali na kuzindua mpango kabambe pia alifanya ukaguzi
katika mifumo ya ukusanyaji wa kodi ofisi za ardhi za halmashauri ya
manispaa ya Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi ya ardhi
yanafanyika kwa malengo mahususi.
Aidha,
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego akiongea na wananchi mbele ya
Waziri Lukuvi, alimhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa atasimamia
utekelezaji wa mpango kabambe kikamilifu kwa maendeleo ya watu wa Mtwara
na watanzania kwa ujumla.
Katika
uzinduzi huo Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji, Bi.
Imaculate Senje ameeleza kuwa uzinduzi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa
kupunguza au koundoa kabisa tatizo la migogora ya ardhi mkoani mtwara,
na kuchochoea fursa za uwekezaji, hivyo amewapa rai wananchi wa Mtwara
kufuata mpango huo kwa maendeleo ya taifa.
Pia
Ndugu Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa ya Mtwara ameeleza
kuwa dira ya mpango kabambe huo ni kuwa na mji mahiri wenye uchumi wa
mafanikio ambao hutoa kazi na fursa za kutosha na kuvutia uwekezaji.
Afisa
huyo ameeleza mpango huo umegusa maeneo ya Naumbu, Mjimwema, Nanguruwe
na Ziwani ukigusa huduma zote za kijamii ikiwemo shule na hospitali na
shughuli za kiuchumi yakiwemo maeneo ya viwanda na uwekezaji.
EmoticonEmoticon