Bibi kizee nchini Mexico akusudia kusoma elimu ya sekondari baada ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi akiwa na miaka 100.

151284_23

 

Bibi mmoja nchini Mexico amefanikiwa kuhitimu elimu ya shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 100.

Bibi huyo Manuela Hernandez (pichani) ambaye alizaliwa katika jimbo la Oaxaca mnamo mwezi Juni 1913, aliacha shule ya msingi baada ya kusoma kwa mwaka mmoja tu na kurejea kuisaidia familia yake masikini kufanya kazi za nyumbani.

Hata hivyo alirejea shule kuendelea na masomo mwezi Oktoba mwaka uliopita akiwa na miaka 99 kufuatia kushauriwa na mmoja wa wajukuu zake.

Manuela-Hernández-a-los-100-años-terminó-la-primaria-Foto-Cba24N

Manuela Hernandez akiwa ameshikilia cheti chake cha kuhitimu elimu ya msingi.

Hivi sasa tayari amekabidhiwa diploma yake ya elimu ya msingi katika sherehe iliyofanyika katika jimbo Mexico Kusini.

Bibi Hernandez amesema sasa ataendelea na masomo ya elimu ya sekondari.

Zaidi ya nusu ya wakazi wa jimbo la Oaxaca wenye umri wa zaidi ya miaka 15 hawajamaliza elimu ya msingi.

Previous
Next Post »