![]() |
Hii ndiyo hali ya Ulinzi wa Mkenya Barack Obama White house Marekani |
Hii ndege itakayosafirisha Magari na Mizigo wakati wa Ziara ya Obama Tanzania Mwezi Ujao.
Humo gari la Msafara wa Obama likiwa Ndani ya Ndege ya Kusafirishia Mizigo Hiyo
RAIS wa Marekani, Bw. Barack Obama, atakuwa na ujumbe wa watu 700 katika ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, aliyasema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema kutokana na ziara ya kiongozi huyo, alitoa wito kwa wafanyabiashara wenye hoteli, migahawa, magari ya kukodisha waziboreshe biashara zao ili Wizara hiyo iingie mkataba nao.
Aliongeza kuwa, akiwa nchini, Bw. Obama atafanya mkutano na viongozi wa nchi zinazoendelea kwa kuzungumzia umuhimu wa sayansi na teknolojia katika nchi zao.
“Ugeni huo ni mkubwa, ujio wa kiongozi huyu utaisaidia nchi kupata pesa
za Miradi ya Changamoto za Milenia (MCC), ambazo zitatumika katika maji, elimu na barabara.
“Pia Rais Obama atazungumzia jinsi nchi za Afrika zitakavyopata umeme wa kutosha tofauti na sasa...kimsingi tumejiandaa katika mapokezi yake hata kwenye mavazi,” alisema Bw. Membe.
Hata hivyo, Bw. Membe alisema tayari baadhi ya ujumbe ambao ataongozana nao umeanza kuwasili nchini kwa matayarisho.
EmoticonEmoticon