Wananchi Afrika Kusini wakesha wakiimba na kumuombea nafuu Mzee Nelson Mandela.

 

28pray4

Wananchi wa Afrika Kusini wamekesha wakimuombea afya njema rais wa zamani wa nchi hiyo mzee Nelson Mandela nje ya nyumba yake ya zamani katika kitongoji cha Soweto.

Kundi kubwa la wananchi hao ilikuwa ikiimba na kumuomba Mwenyezi Mungu ampe nafuu Mzee Mandela, ambaye amelazwa kwa 20 katika hospitali mjini Pretoria na hali yake imeelezwa kuwa mbaya  lakini  imara.

Rais Jacob Zuma wan chi hiyo amemtembelea Mzee Mandela mwenye umri wa miaka 94 na kueleza kuwa hali yake imeanza kuimarika lakini bado yu mahututi.Rais Zuma ameahirisha ziara yake nchini Msumbiji ambako angehudhuria mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Previous
Next Post »