Meshack Maganga-Iringa.
Katika makala zangu huko nyuma nilipata kuandika
makala moja niliyoipa kichwa cha KWENYE UJASIRIAMALI NG'OMBE WA MASKINI HUZAA
nilizungumzia na kukanusha juu ya imani potofu isemayo 'NG'OMBE WA MASKINI
HAZAI', nilisema kuwa, kwenye ujasiriamali ni kinyume chake, kwamba Ng'ombe wa
maskini anaweza kuzaa tena mapacha. Nilielezea kwa kirefu jinsi ambavyo baadhi
tunapokuwa tumetafuta mitaji, na kuhangaika hapa na pale na ikatokea muda
mwingi umepita bila kufanikiwa huwa tuna kata tama na kuanza kutamka maneno na
methali kama hiyo hapo juu.
Nilieleza kwamba kuna kanuni vichwani mwetu na
tunaweza kuitumia katika kutupatia hamasa ya kuwa wajasiriamali wakubwa na bora
kuliko wote hapa duniani.Leo nianze kwakusema kwamba, binadamu ana mambo matatu
muhimu ambayo anaweza kuyaendesha au yakamwendesha kichwani kwake, moja ni
fikra zake au mtazamo(thoughts you think),mbili ni taswira anazozijenga
kichwani kwake(image you visualize) na tatu ni vitendo vyake (the actions you
take).Sisi binadamu tunawajibu wa
kuhakikisha tunaleta maendeleo katika maeneo
tunayoishi kwa juhudi zetu binafsi. Ni kweli tumesikia na kujifunza mengi
katika dunia lakini maana ya maisha iliyo halisi na ya kweli ya mwanadamu
mhusika hutoka ndani ya binadamu mwenyewe. Kila mwanadamu anao ukweli wa maisha
yake ndani yake.
Mambo yote tunayoyaona duniani, ugunduzi, vitabu,
miziki, filamu na kila kitu kilichopo duniani kilichosababishwa na mwanadamu
asili yake ni ndani ya binadamu na si nje. Ndani yako mwanadamu kuna maajabu,
ndani yako kuna hazina ya maisha, vipaji, talanta na habari njema ya maisha
yako.
Kutokana na upekee ulionao duniani, huna
mshindani, mshindani wako ni wewe mwenyewe.Historia ya dunia inaonyesha kuwa
wanadamu walio wengi duniani wanafichwa mambo ya ukweli na makubwa kuhusu uwezo
wao.
Toka enzi za wajasiriamali tunaowasoma katika
historia akina Adam Smith, kipindi cha viwanda na utumwa wanadamu wengi,
waliishi chini ya viwango kwa kutumika kama mashine zinazoweza kubadilishwa
wakati wowote, hii imekuwa sababu kubwa ya binadamu wengi kutokujua ukweli wa
vipawa ndani yao na hata kutojiamini kabisa.
Vilevile Kutokana na mabadiliko ya maisha, karne
hii ya 21 inatabiriwa kuwa karne ya vipawa na maajabu ya ndani ya mwanadamu
kwani imedhihirishwa na baadhi ya watu wa kawaida sana ambao wameweza kugundua
mambo mengi kwa kutumia vipawa vyao.
Tunaishi katika dunia ambayo ni rahisi kubebwa na
misukumo ya nje na wengi hawaamini ukweli huu kuwa kila mtu ana kipaji, kila
mtu ana habari njema ya ndani yake hii ni kwasababu wengi wameshawishiwa na
mifumo ya dunia na maisha ya wanadamu wengine na kujikuta kuwa wanaishi si kama
wao bali kama nakala.
Watu wote wenye mafanikio duniani, ambao
huonekana kana kwamba wamebarikiwa hutafuta maana ya wao kuwa wao, uwezo wao wa
kipekee na kutumia upekee walionao na kuishi maisha yao kimafanikio watakavyo
wao.
Dunia hii inayo nafasi kwa mwanadamu ambaye
anatafuta maana ya maisha yake mwenyewe, haijalishi umezaliwa katika familia ya
aina gani bali ukikubali ukweli kuwa unayo hazina ya maisha ndani yako basi
maisha yako yatapata maana.
Unacho kipaji ndani yako.Hakuna mwanadamu ambaye
hakuumbwa na kitu ndani yake, Mungu hakuumba takataka duniani, Mungu aliumba
mwanadamu mwenye hazina ndani yake. Kila mwanadamu anao uwezo wa kipekee na
kiasili aliojaliwa na Mungu ambao bila yeye hakuna ukamilifu. Uliletwa duniani
ili ukamilishe upekee wako. Wewe ni ukamilifu wa dunia, kuishi kama nakala
haina tofauti na kuishi kama marehemu anayetembea.
Unaweza usiwe na uwezo kuanzisha biashara ya
mgahawa au ya daladala lakini ukawa na uwezo wa kuimba na kutunga nyimbo za
kila aina hivyo ukawa mjasiriamalia katika kanda ya mziki iwapo una uwezo wa
kuchekesha basi fanya ujasiriamali katika kipengele cha ucheshi kama jamaa wa
futuhi.
Wapo walioletwa duniani ili kuifanya dunia
icheke, wapo walioletwa duniani ili kuifanya dunia icheze,wapo walioletwa
duniani ili kuifanya dunia itembee, wapo walioletwa duniani ili kuifanya dunia
ifikiri, wapo walioletwa duniani ili kuifanya dunia isikilize radio,TVs na
muziki, wapo walioletwa duniani ili kuifanya dunia ing'are na mengine mengi
unayoyajua na ambayo mpaka sasa hatujayajua bado lakini yamo ndani yako. Aidha
wapo walioletwa duniani ili kuifanya dunia iwe na mitandao tunayoiona sasa
hivi.
Dunia hii inakuhitaji wewe kama wewe, na
mafanikio yako duniani yanakutegemea wewe kama wewe. Hata kama usipokubali
ukweli wa uwezo wako wa ndani, haitaondoa maana ya ukweli ulio ndani yako.
Kumbuka kuwa utamu wa maisha duniani ni matumizi ya kipaji chako na kusikiliza
sauti ya ndani.Ulipewa vipaji ili uvitumie duniani katika
biashara,kazi,sanaa,uongozi,ujuzi,masomo na mengine.
Bila kujionea aibu mwenyewe, na kujitafuta na
kujiuliza kasoro zako ulizonazo na jinsi ya kuzizuia au kuzipunguza, tafuta
kujua mazuri ya kwako huku ukitafuta kuongeza mengine. Ukiona Kama kuna kitu kinakufurahisha
duniani, usiogope kujaribu, jaribu, jaribu tena ipo siku utagundua wewe ni
mzuri wapi.
Sikiliza zauti za dunia lakini sikiliza sana sana
sauti yako ya ndani kwani ndiko kutokako chemchem ya uhai wa maisha yako.
Jifunze kujiuliza, wewe ni nani? Umetoka wapi? Una nini cha kujivunia duniani?
Unataka dunia ikukumbuke vipi? Je uko tayari kuja duniani kama moshi na
kuondoka kama moshi, usikumbukwe? Nini unaweza zaidi ya mwingine? Ni nini
madhumuni yako duniani?
Kumbuka kuwa wewe ndiye mkurugenzi mtendaji wa
maisha yako, mazingira, mifumo, familia na vikwazo vyovyote duniani visiwe
sababu ya kuutuliza utu wako. Unazo nguvu zaidi ya nguvu zilizo nje yako za
kuwa unavyotaka, kulingana na jinsi ulivyojaliwa. Vipo vitu vinavyoweza
kukuzuia hata kukumaliza lakini ni uamuzi wako kusimama kidete kwaajili ya
maisha yako na kuonyesha nguvu zilizo ndani yako au kukubali kumalizwa bila
ubishi wowote.
Vipo vitu vingi vinavyoweza kukuchanganya. Lakini
ni uamuzi wako kukubali kuchanganywa na kuishi maisha ya bora liende au ili
mradi kumekucha mpaka unakufa bila maana au kuamua maisha yako na kusema ama
zangu ama zao nitakuwa vile ninavyotaka maishani.
Kumbuka kuwa dunia haina huruma kwa mwanadamu
aliyekubali kumalizwa, vumilia, jiamini, Jipende, jiendeleze, jikaze,
jionyeshe, jitafute mwenyewe, jikubali na mwisho wa siku dunia itakukubali tu
hata kama kuwe na nguvu zozote mbele yako.
Kumbuka kuwa dunia hii itaendelea kuendeshwa na
hata kutengenezwa na binadamu wenye uelewa mpana wa nguvu iliyo ndani yao na si
wababaishaji na wenye maisha ya maridadi.Wanadamu wote walioweza kufanikiwa.
Juzi kuna rafiki yangu anaye soma katika moja ya vyuo vikuu hapa Iringa, alikuja ofisini kwangu na kuniuliza "unanisahuri nikimaliza masomo yangu ni fanye kazi katika kampuni gani"? mwanzo nilishangaa msomi wa chuo kikuu akiuliza swali hilo,nilitambua kwamba kuna umuhimu wa wanafunzi kufundishwa somo la utambuzi ili wafahamu vipaji vyao.Hasa kwa vile watanzania hawana utamaduni wa kujisomea makala na vitabu vya utambuzi na maarifa na siyo wanafunzi tu,ni pamoja na walimu wao na wahadhiri wao na viongozi kwa ujumla, anaye pinga aniambie.
Tunachoweza ni kulaumu watu wasiohusika katika maisha yetu magumu, kuwa wanaharakati wa mambo yasiyotuhusu,kutoa maoni yasiyo na maoni na kuchambua timu za ulaya na kuelezea mchezaji fulani analipwa kiasi gani cha mshahara.Ni lini umewahi kaa nyumbani kwako au kwenu na ukatumia muda wako kuchambua vipaji vyako? Ambavyo ungevitumia katika maisha yako na jamii inayokuzunguka?
Juzi kuna rafiki yangu anaye soma katika moja ya vyuo vikuu hapa Iringa, alikuja ofisini kwangu na kuniuliza "unanisahuri nikimaliza masomo yangu ni fanye kazi katika kampuni gani"? mwanzo nilishangaa msomi wa chuo kikuu akiuliza swali hilo,nilitambua kwamba kuna umuhimu wa wanafunzi kufundishwa somo la utambuzi ili wafahamu vipaji vyao.Hasa kwa vile watanzania hawana utamaduni wa kujisomea makala na vitabu vya utambuzi na maarifa na siyo wanafunzi tu,ni pamoja na walimu wao na wahadhiri wao na viongozi kwa ujumla, anaye pinga aniambie.
Tunachoweza ni kulaumu watu wasiohusika katika maisha yetu magumu, kuwa wanaharakati wa mambo yasiyotuhusu,kutoa maoni yasiyo na maoni na kuchambua timu za ulaya na kuelezea mchezaji fulani analipwa kiasi gani cha mshahara.Ni lini umewahi kaa nyumbani kwako au kwenu na ukatumia muda wako kuchambua vipaji vyako? Ambavyo ungevitumia katika maisha yako na jamii inayokuzunguka?
Kwa kujitengenezea mafanikio wenyewe kutoka chini
ni wale ambao wametambua sababu ya wao kuwa wao, wanajijua ni nini wanakitaka
na wanajua kuwa ili maisha yao yawe na maana lazima wafanikiwe.
Maisha ya mafanikio duniani ni haki ya kila
mwanadamu. Hakuna binadamu aliyeletwa duniani kuja kushuhudia wengine
wakifanikiwa huku yeye akiwa katika umaskini siku zote. Kila mwanadamu mwenye
pumzi anayo haki, nafasi, uwezo na uchaguzi wa kuwa anavyotaka kulingana na
maana ya mafanikio atakayotengeneza na mwenyewe.
Ni kweli tunaishi katika dunia yenye utofauti
kimafanikio wapo wenye mafanikio makubwa, wapo maskini na wale wenye maisha ya
kawaida. Lakini kwa pamoja yatupasa tufahamu kuwa, kila mwanadamu anao uwezo wa
kufanikiwa.
Na zaidi ni kuwa kila mtu anao uchaguzi wa kuamua
maisha yake, lakini angalizo ni kuwa mtu yeyote aliyeweza kufanikiwa ametambua
kuwa , kuna vichangizi vya
mafanikio / success ingredients.
mafanikio / success ingredients.
Unachopaswa kutambua ni kuwa, hali ya maisha
uliyonayo sasa si kipimo cha mafanikio yako ya baadaye, unaweza kuwa vyovyote
kimafanikio kulingana na utakavyochagua mwenyewe. Ni muhimu kuyajua maisha Kwa
kujua vipaji na vichagizi hivyo ni kama vifuatavyo:
Mwanadamu anayejua dhumuni lake duniani huishi
maisha ya maana. Hatukuja duniani kuwepo tu bali kuishi kimafanikio huku
tukijua kwanini tunaishi. Ukijua ni kwanini unaishi hutakubali kuishi
kiholelaholela huku ukisubiri muda wako wa kuishi duniani kuisha.
Dhumuni la wewe kuwepo duniani ni kuishi maisha
yenye madhumuni, maisha yenye mafanikio na maisha yanayonufaisha wengine.
Wanadamu wote walioweza kufanikiwa kwa kujitengenezea mafanikio wenyewe kutoka
chini ni wale ambao wametambua sababu ya wao kuwa wao, wananjua ni nini
wanakitaka na wanajua kuwa ili maisha yao yawe na maana lazima wafanikiwe
katika hilo.Ukitaka kutengeneza maisha yenye mafanikio duniani, tafuta kujua
dhumuni lako hapa duniani.
Wanadamu wote waliofanikiwa duniani waliamini
kuwa wanaweza kuibadili dunia. Mwanadamu anayeyarudisha maisha yako nyuma ni
wewe mwenyewe, ukitaka kufanikiwa katika lolote utakalochagua jiamini na amini
kuwa unaweza. Hakuna kitu chochote kilichowahi kutokea duniani bila kujiamini.
Kila mwanadamu anayo zawadi ndani yake, zawadi
hii huja kama kitu anachokipenda na kukiweza. Ndani ya mwanadamu vipo vipawa na
uwezo wa ajabu wa kuishi maisha ya mafanikio. Kila mtu ana kitu anachopenda,
kinachoweza kutumika na kuendelezwa na kuleta mafanikio.
Dunia ya sasa ni dunia ya wanadamu wanaojua ni
kitu gani wanaweza. Wapo wanaopenda kuwa madaktari, wapo wanaopenda kuwa
waimbaji nk. Kila mtu ana kitu anachopenda kinachomfanya acheke akiwa duniani.
Tafuta kitu unachokipenda na kiendeleze, kitakuletea mafanikio.
Maisha ni vitendo na si ndoto pekee, ndoto ni
mwanzo tu wa maisha. Maisha ni kuchukua hatua na si kufikiri pekee. Maisha ya
kijasiriamali ni kusonga mbele na si kupanga peke yake. Katika yote uliyochagua
maishani kuwa mtendaji, usikubali kuyaishi maneno ishi matendo.
Maisha bila maarifa ni sawa na gari lisilo na
mafuta. Ukitaka kutembea na kuishi kimafanikio kuwa na njaa ya maarifa kila
siku. Binadamu wote wenye mafanikio duniani hawachoki kutafuta maarifa kwa
kusoma vitabu, kuuliza na kujifunaza, na hata kuhudhuria mafunzo ya
kuwaendeleza mara kwa mara. Maisha bila maarifa hayatembei.
Maisha yana mengi, muda mwingine yale tunayapanga
hayaji kama tulivyopanga lakini yote hutokea kwasababu. Mambo yote tunayapitia
katika maisha huwa ni hatua ya ukuaji kimaisha. Ukiona biashara yako inafanya
vizuri tambua kuwa ni kweli biashara yako inakua, lakini ukiona biashara yako
inafanya vibaya tambua kuwa uwezo wako unakua zaidi.
Nahitimisha kwa kusema kila mtu ana uwezo wa
kuchagua kuwa mjasiriamali wa kipekee na yale ayatakayo maishani, Dunia ina
mengi ya kuyafanya na kuna kila nafasi kwa mwanadamu yeyote anayechagua kuwa
anavyotaka maishani. Chagua maisha unayotaka kuyaishi na uyaishi kweli.
Usiogope kujaribu kitu, maisha ya kuogopa kufanya
kitu ni maisha yasiyo na maana. Usikubali maisha ya ukawaida na yenye usalama
ambayo yatakufanya usiishi maisha makubwa unayostahili.
Siri kubwa ya watu wenye mafanikio duniani, ni
kuwa hawaogopi maisha, wapo tayari kuumia kwa kuchagua maisha wayatakayo.
Chagua kipengele mojawapo cha kijasiriamali unachotaka kukifanya na ukifanye
kweli kwa moyo wote. Jiendeleze kila siku katika ulilochagua kiasi ambacho
utavunja mipaka na kuweka rekodi yako. Chagua kufanikiwa
EmoticonEmoticon