Kufuatia tamko hilo tayari marubani wameshapelekwa nchini Canada kwa ajili ya mafunzo ya kurusha ndege hizo zitakazowasili nchini mwezi Septemba. Kufuatia ujio huo wa ndege mbili, ATCL inatarajia kuajiri wafanyakazi 28 watakaohudumu katika ndege hizo mbili.
Mchanganuo wa wafanyakazi hao ni kama ifuatavyo;-
- Shirika la Ndege (ATCL) litaajiri marubani wanne, ambao ni sawa na marubani wawili kwa kila ndege moja kwa ajili ya kurusha ndege hizo.
- Shirika la Ndege (ATCL) litaajiri wahandisi sita ambao ni sawa na wahandisi watatu kwa kila ndege moja. Hawa watashungulika na matengenezo ya ndege pindi inapokuwa na tatizo.
- Shirika la Ndege (ATCL) litaajiri wahudumu 18 ambao ni sawa na wahudumu tisa kwa kila ndege. Hawa watakuwa wakitoa huduma kwa abiria pamoja na maelekezo mbalimbali kuhusu ndege wakati wa safari.
EmoticonEmoticon