Idris alieleza kukerwa na tabia ya Wema Sepetu kutoonekana kwenye show zake angali yeye amekuwa mstari wa mbele kila anapokuwa na show anakwenda.
Kabla ya kuifunga akaunti yake iliyokuwa na wafuasi (Followers) zaidi ya milioni 1, Idris aliandika maneno haya;
“Sipendi kuona watu wakiingia na kuongea kama wanajua maisha yangu na watu wangu wa karibu, makosa wakifanya wengine mnakuja kwangu mnaanza “Ndio asingefanya vile kama sio wewe kufanya hivi” mnakazana kusema eti naposti wanawake mara ooo porojo kibao. Sina freedom ya kumpost dada angu ? Kweli ? Au rafiki yangu kazindua brand mpya siwezi mpost nikampongeza?.”
“Mnauliza kwanini sijaenda vigoma nimesema because show yangu hakuja hata moja na nimeenda show zake zote na yeye halalamiki because anajua nimesema siendi fair enough mbona hamjaongelea hilo? I repeat nikikaa kimya is for a pure reason that it’s not anyones business this is my personal life kama mnaongeleaga fair basi mngefanya kuuliza kwanini mpaka am selling out hajaja,”
“Give me a break sina maisha ya kuigiza lets have respect for each other bana. Na nimesema msiniite shemeji for one big good reason, imekua too much i am a brand na jina idris linamezwa na shem, ningejua this from the beginning nisingeruhusu mniite tangu mwanzo so msiwe kila kitu mnafikiria negative tu. Na sikuwa na haja ya kuandika yote haya pia TusichukulianePoa.”
Kuna taaarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wema Sepetu na Diamond sasa wamerudiana japo ni kwa siri kubwa. Hii huenda ikawa ni sababu ya Idris kupigwa cha mbavu na mrembo huyo.
EmoticonEmoticon