Rubani wa Ukraine jela miaka 22 Urusi
Rubani kutoka Ukraine anayetuhumiwa kwa mauaji ya wanahabari wawili kutoka Urusi amehukumiwa kifungo cha miaka 22 gerezani.
Nadiya
Savchenko alipatikana na hatia ya kufyatua makombora yaliyowauwa
wanahabari hao waliokuwa wakipeperusha habari kutoka eneo la vita vya
wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la Ukraine na waasi wanaotaka
kujitenga wanaoaminika kuungwa mkono na Urusi.
Kisa hicho kilitokea mwezi juni mwaka wa 2014.
Savchenko aliangua kicheko punde baada ya majaji hao kumaliza kusoma hukumu yao.
Alianza kuimba nyimbo za kitamaduni za kizalendo kama njia yake ya kupinga uamuzi huo.
Savchenko alikanusha madai dhidi yake.
Nadiya Savchenko alipatikana na hatia ya kufyatua makombora yaliyowauwa wanahabari 2 wa Urusi
Mara
baada ya hukumu hiyo kutolewarais wa Ukraine Petro Poroshenko alipuzilia
mbali uhalali wake na kusema kuwa yuko tayari kubadilisha rubani huyo
shupavu na wanajeshi wawili wa Urusi waliokamatwa.
Aidha waziri wa maswala ya kigeni wa Ukraine aliahidi kuendelea na harakati za kutafuta uhuru wa rubani huyo.
Kulitokea makabiliano baada ya mashabiki wa rubani huyo kujaribu kupeperusha bendera ya Ukraine ndani ya mahakama.
Kiongozi
wa mashtaka alisema kuwa bi Savchenko alikuwa na chuki sana dhidi ya
Urusi na hiyo ndiyo iliyompelekea kuwashambulia waandishi habari
hao,.ambao hawakuwa wamejihami.
Kesi hiyo iliendeshwa katika mji wa mpakani wa Donetsk.BBC
EmoticonEmoticon