STARTIMES YATOA MSAADA WA IPAD KWA WIZARA YA HABARI


T1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Nnauye ( katika) akisalimiana na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing wakati alipowasili katika ofisi za Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes kwa ajili ya kupokea msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini, kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang.
T2
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Nnauye kabla ya sherehe za makabidhiano ya  msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini toka Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes, mapema jana jijini Dar es Salaam.
T3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akiteta jambo na Kaimu Mkurugezi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa wakati wa sherehe za makabidhiano ya  msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini toka Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes, mapema jana jijini Dar es Salaam (katikati) ni Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba.
T4
Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang (katikati) akimtambulisha Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba kwa (kushoto) kwa Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu You Qing wakati wa sherehe za makabidhiano ya  msaada wa iPad kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Maafisa Mawasiliano Serikalini toka Kampuni ya ving’amuzi ya StarTimes, mapema jana jijini Dar es Salaam.
Previous
Next Post »