Waziri
wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza
katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu kumsimamisha kazi Mtendaji
Mkuu na Wakurugenzi watatu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House
Jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya
Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani.
Baadhi ya
Waandishi wa habari Waliohudhuria Mkutano huo wa Waziri wa Maliasili na
Utalii Prof. Jumanne Maghembe katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu
wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa
Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na
Waandishi wa Habari kuhusu kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu na
Wakurugenzi watatu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika
ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar
es Salaam jana.
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa
Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Mghembe amemsimamisha kazi Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini, (TFS) Bw. Juma Mgoo
pamoja na Wakurugenzi wawili wa wakala hiyo ili kupisha uchunguzi
kutokana na ukusanyaji usioridhisha wa mapato yatokanayo na mazao ya
misitu.
Prof.
Maghembe ametaja majina ya Wakurugenzi hao aliowasimamisha kazi kuwa
ni Mkurugenzi Rasilimali Misitu, Bw. Zawadi Mbwambo pamoja na
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi endelevu ya Misitu, Bw.
Nurdin Chamuya
Wengine
waliosimamishwa kazi ni wakuu wa Kanda za Wakala wa Huduma za Misitu
nchi nzima ambao ni Bw. Hubert Haule wa Kanda ya Kusini, Bw.
Bakari Rashidi wa kanda ya Mashariki, Bw. Shabani Mwinyi Juma wa kanda
ya kati , Emanuel Minja wa kanda ya Magharibi pamoja na Bw. Bruno wa
nyanda za juu kusini
Akizungumza
jana na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es
Salaam, Prof. Maghembe amesema hatua hiyo imekuja baada ya kubaini
shehena kubwa za magogo aina ya mninga katika Mkoa wa Rukwa wilayani
Kalambo yakiwa yamekatwa na kuwekwa ndani ya makontena kule kule
ndani ya msitu pamoja na kutengenezewa nyaraka feki zinazoonesha
magogo hayo yanatoka nchini Zambia tayari kwa kusafirishwa
kupelekwa nchini China lakini hata hivyo baada ya kubaini wizi huo
hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na Wakala ya Huduma za Misitu
Tanzania ( TFS).
Amesema
kuwa baada ya kubaini hivyo usiku wa jana aliweza kupata taarifa kuwa
shehena ya Magogo hayo yenye thamani ya shilingi milioni 500
yaliyotakiwa kupelekwa Makao makuu ya Wilaya ya Kalambo yamemwagiwa
petrol na yamechomwa moto
Aliongeza
kuwa kumekuwa na ubadhilifu unaofanywa na Maofisa wa ukusanyaji wa
maduhuri ya Serikali yanayotokana na rasilimali za misitu katika Mikoa
na Wilaya kwa kutowasilishwa katika mfuko Mkuu wa Serikali.
Kwa upande mwingine , Prof Maghembe amesema kuwa pesa zitokanazo na makusanyo hayo zimekuwa hazipelekwi benki kwa wakati na hata zikipelekwa benki zimekuwa zikipelekwa pungufu na muda mwingine pesa hizo zimekuwa hazipelekwi kabisa.
Kwa upande mwingine , Prof Maghembe amesema kuwa pesa zitokanazo na makusanyo hayo zimekuwa hazipelekwi benki kwa wakati na hata zikipelekwa benki zimekuwa zikipelekwa pungufu na muda mwingine pesa hizo zimekuwa hazipelekwi kabisa.
Wakati
huo huo, Waziri Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Wanyamapori wa Matumizi Endelevu, Dkt. Charles Mulokozi kwa
kosa la kukaidi agizo la kusaini vibali vya kusafirisha Wanyamapori
nje ya nchi.
Hatua
hiyo imekuja baada ya jana nyani 61 kukamatwa katika Uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Kilimanjaro na kubaini kuwa Idara ya Wanyamapori ndio
iliyotoa vibali vya kusafirisha nyani hao na vibali hivyo vikiwa
vimetiwa saini na Mkurugenzi huyo.
Ameongeza
kuwa ndege ya kutoka Ulaya Kusini iliyotakiwa kusafirisha nyani hao
imeshikiliwa pamoja na rubani wake kwa mahojiano zaidi.
Prof
,Maghembe amesema kutokana taarifa alizozipata kuwa jumla ya nyani 450
ndio waliokuwa wanawindwa kwa ajili ya kusafirishwa kupelekwa nje.
EmoticonEmoticon