Imeandikwa na Paul Masatu, Dar
Wahenga
walisema “Success is a journey not destination”, mafanikio ni mchakato
unapitia, ni vizuri kuyatazama mafanikio katika namna hii, hii ni rough
road ambayo utakutana na vikwazo vingi ukiwa njiani "Njia iendayo
uzimani ni nyembamba, na wapitao humo ni wachache".
Kwa hiyo
kufikia mafanikio lazima ujue kuna what we call a "price tag" kuna
gharama lazima ulipe ili kufikia mafanikio yako, kuijua ni gharama gani
unatakiwa kulipa, na utayari wako wa kuilipa hiyo gharama vinakupa
nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa.
Bahati
mbaya kizazi tulicho nacho ni kizazi cha miujiza, kinapenda mambo
yatokee ghafla tu from no where, waswahili wanaita "ghafla bin vuu"
hakitaki kabisa kulipa ghalama, mtu anataka alale akiamka tu akute
matatizo yake ya fedha yamekisha, si ajabu katika kipindi chetu hiki
biashara ya utapeli unalipa sana, matapeli wameongezeka sana, ni rahisi
kutapeli watu kwasababu watu hawataki kulipa gharama.
Utakuta
mtu imemchukua miaka kumi kutengeneza matatizo yake ya kifedha au ya
ndoa yake aliyo nayo sasa hivi, lakini cha ajabu anataka hayo matatizo
yaishe by overnight, hiki ni kituko cha a
jabu.
Kuna
tabia mbili kubwa ambazo utaziona kwa watu wasiotaka kulipa gharama
ambao mimi nasema hawa qualify kufanikiwa. Tabia hizo ni
a)
wanapenda sana "Instant gratification" yaana wao maisha ni sasa tu,
hawaangalii kesho, wako tayari kuharibu hatima yao kwa raha za muda,
hawako tayari kuvumilia maumivu kidogo ili waweze kutengeneza kesho bora
zaidi, hawa wamesahau ule msemo wa kingereza unaosema " No gain without
pain"
b) Tabia
ya pili ambayo ni most common kwa unsuccessful people wengi wanakuwa na
short term vision" yaani hawaoni mbali kabisa, wao maisha ni sasa hivi
tu, wanashindwa kujizuia kwasababu wanashindwa kupiga picha na kuona,
hiki ninachofanya sasa hivi madhara yake ndani ya mwezi, au mwaka au
miaka mitano itakuwaje??
Lakini vile vile utafiti unaendelea na kugundua sifa mbili kubwa ambazo zinapatikina kwa watu wengi waliofanikiwa. Sifa hizo ni
a) Delayed gratification
Yaani wako tayari kujizuia mambo fulani, kwa ajili ya faida yakesho, kwa maneno mengine yuko tayari kulipa gharama, yuko tayari kuvumilia kwa kujitoa kukomalia jambo fulani, hata kama kuna some pain, ilimradi afanikishe lengo lake, yuko tayari kujizuia mambo mambo fulani yanayo mchukulia hela sana, ilimradi aweze ku save na kufanikisha lengo lake.
Yaani wako tayari kujizuia mambo fulani, kwa ajili ya faida yakesho, kwa maneno mengine yuko tayari kulipa gharama, yuko tayari kuvumilia kwa kujitoa kukomalia jambo fulani, hata kama kuna some pain, ilimradi afanikishe lengo lake, yuko tayari kujizuia mambo mambo fulani yanayo mchukulia hela sana, ilimradi aweze ku save na kufanikisha lengo lake.
...Nitaendelea
EmoticonEmoticon