JWTZ LIMESEMA HALI YA MAJERUHI MMOJA KATI YA 14 WALIOSHAMBULIWA NA WAASI DARFUR IMEZIDI KUWA MBAYA


 


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema hali ya majeruhi MMOJA kati ya 14 walioshambuliwa na waasi huko Darfur, Nchini SUDAN wakati wakisindikiza Waangalizi wa Umoja wa Mataifa imezidi kuwa mbaya.
Akizungumza na Clouds FM, Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali KAPAMBALA MGAWE amesema kutokana na hali hiyo majeruhi huyo amepelekwa Khartoum nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi huku wengine tisa wakitajwa kuaendelea vizuri.
Katika hatua nyingine Kanali MGAWE amewataka Wananchi kuepuka taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa katika Mitandao mbalimbali kuhusiana na hali ya majeruhi hao
Previous
Next Post »