NAFURAHISHWA SANA NA JITIHADA ZA DADA DINA MARIOS KEEP IT UP MDADA

 

 

DADA DINA CARES NA WATOTO YATIMA WA ZAIDIA SINZA.

Jumatatu ya tarehe 5 august tuliwasilisha vitu kwa watoto wa Bi Zaidia Sinza.Bahati nzuri kuna kikundi cha akina mama kinaitwa shekilango women group walikuja kuungana nasi kwa ajili ya kutoa chochote kwa watoto.
 Tulifika na wakina mama walipata wasaa wa kujitambulisha kwa mwenyeji wao na kuongea na watoto.
 Shilole nae alikuja kushiriki na alizungumza na watoto.Shilole nae ni yatima.
 Gea Habib na mie tukimwangalia shilole wakati akiongea
 Watoto tuliwakuta baadhi wengine walikuwa shule.Wana adabu hao na wastaarabu sana.
 Mama alisali sala maalum ya kuwaombea watoto na wageni.
 Vitu tulivyowaletea
Mwenyeji wetu mama Zaidia alitushukuru na kuomba dua maalum kwa wageni wote na wote mlioshiriki kufanikisha hili.Baada ya hapo tuliondola na kwenda kuendelea na ratiba zingine za siku.Bado naendelea kushukuru wooote mlioshiriki kuchanga na kufanikisha mpango huu.
Previous
Next Post »