·
MTU MMOJA MKAZI WA ISANGA JIJINI MBEYA AFARIKI
DUNIA WAKATI AKIPATIWA MATIBABU BAADA YA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI.
·
JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
WANNE KWA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA MKAZI
WA ISANGA JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EMANUEL MICHAEL @ ZAWADI MICHAEL (30) ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI HUKO ENEO LA MLIMA RELI MBALIZI KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI WA GARI.
AWALI MNAMO TAREHE 15.04.2015 MAJIRA YA SAA 03:30 ALFAJIRI HUKO KATIKA ENEO LA
NSALAGA – UYOLE, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA,
MAREHEMU EMANUEL MICHAEL @ ZAWADI MICHAEL
ALIVUNJA MLANGO WA NYUMBA YA BWANA PHILIPO
MREMA (34) MKAZI WA NSALAGA NA KUIBA TV AINA YA SAMSUNG, REDIO AINA YA SUB-
WOFFER NA FUNGUO YA GARI NA KISHA KUIBA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.828 BQG
AINA YA TOYOTA CARINA RANGI YA SILVER NA KUTOKOMEA KUSIKOJULIKANA.
KUTOKANA NA
TUKIO HILO, MSAKO MKALI ULIENDELEA WA KUMTAFUTA MTUHUMIWA NA MNAMO TAREHE 15.04.2015 MAJIRA YA SAA 07:00 ASUBUHI HUKO ENEO LA MLIMA RELI MBALIZI WILAYA YA
KIPOLISI MBALIZI, MAREHEMU ALIKAMATWA NA KUSHAMBULIWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA
WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI HALI ILIYOPELEKEA KUTOKWA DAMU
NYINGI NA ALIFARIKI WAKATI ANAPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
CHANZO CHA TUKIO
HILI NI KIPIGO NA KUTOKWA DAMU NYINGI BAADA YA KUKUTWA NA GARI HILO LA WIZI
AMBALO ALIKUWA AMEANZA KULICHOMA MOTO KUTOKANA NA KUSHINDWA KUTOKOMEA NA GARI
HILO BAADA YA KUPATA HITILAFU. AIDHA TAARIFA ZINADAI KUWA, MAREHEMU ALIKUWA
MWIZI MZOEFU WA MAGARI NA ALIPOPEKULIWA ALIKUTWA NA LESENI YA UDEREVA, FLASH NA
SIMU MALI YA MLALAMIKAJI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TAMAA YA MALI/UTAJIRI WA HARAKA KWA NJIA
ZISIZOHALALI NA BADALA YAKE WAJIHUSISHE KATIKA SHUGHULI HALALI ZA KUJIPATIA
FEDHA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA MKAZI WA IPINDA WILAYANI KYELA ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA HURUMA ADAMSON (23) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA ISHIRINI
[20] AKIWA AMEHIFADHI KWENYE DUMU.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.04.2015
MAJIRA YA SAA 18:40 JIONI HUKO
KATIKA ENEO LA STENDI YA MABASI KYELA MJINI, KATA YA KYELA-KATI, TARAFA YA
UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA TUSA TUSAJIGWE (23)
AKIWA NA BHANGI UZITO WA ROBO KILO.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.04.2015
MAJIRA YA SAA 13:30 MCHANA HUKO ENEO
LA ILOMBA, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI MTUHUMIWA ZINAENDELEA.
KATIKA
MSAKO WA TATU, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ATUPELE MPOTA
(49) MKAZI WA KATUMBA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MBILI [02].
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.04.2015
MAJIRA YA SAA 18:40 JIONI HUKO
KATIKA ENEO LA KATUMBA, KATA YA IBIGI, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA
WA MBEYA.
KATIKA
MSAKO WA NNE, JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA KIJANA MMOJA
MKAZI WA KIJIJI CHA KYIMO WILAYANI RUNGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KELVIN AJERO (19) AKIWA NA SIGARA AINA
YA SWEET MENTHOL (SM) BUNDA 17 ALIZOINGIZA NCHINI KWA MAGENDO KUTOKA NCHI JIRANI YA ZAMBIA.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE
15.04.2015 MAJIRA YA SAA 14:35 MCHANA
HUKO KATIKA ENEO LA KATUMBA, KATA YA IBIGI, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE,
MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA WOTE ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KABISA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA, POMBE HARAMU YA MOSHI NA KUJIHUSISHA NA
BIASHARA YA UINGIZAJI NA USAMBAZAJI WA BIDHAA KINYUME CHA SHERIA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon