SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?SEHEMU YA SABA.

Displaying 20150416_095124-BlendCollage.jpg

MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA

Sim no,0755683295/Watsap. Email@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala,Instagram @mwalim_yuu.

SEHEMU YA SABA.
Tulipoishia Nikaingia chumbani huko ndo ilikua matatizo. Kwanza niliona mke wangu ametoka povu jingi mdomoni. Pia nilimwona mwanangu wa kumzaa Ametapakaa damu na kichwa kimekatwa. Nilipigwa na butwaa. Nikapepesa macho yule mtoto wa bosi sikumwona. Ghafla______Endelea.... Nikasikia kama kisauti chamtu mwenye woga. Kilikua kinatokea kabatini. Nikafungua kabati kwa nguvu mlango wa kwanza sikuona kitu. Nikavuta wa pili haa! Nikasikia makelele huku yule mtoto akilia kwa woga. Nikamshika na kumjuza kua ni mimi. Alikua akilia kwa woga akijua labda wabaya bado wapo. Swala likaja je nani anahusika? Aliyeshuhudia mauaji yale alikua ni yule mtoto. Lakini hasikii wala hawezi kuongea. Nilijawa na hasira sana juu ya swala lile.

Nilitoka sebuleni kuona kama kuna chochote lakini sikuona. Nikawapigia simu polisi wenzangu. Wakaja kuangalia walinipa pole lakini ilikua kama kelele masikioni mwangu. Niliumia kuona mke wangu kafa na mwanangu kukatwa kichwa. Ni watu niliokua nawategemea sana katika maisha yangu. Nilimpenda sana mke wangu. Nilimpenda mwanangu. Afande nilidosha machozi pale nilipoona mwili wa mke wangu unapakiwa kwenye difenda. Lakini wakati wanainua ule mwili chini niliona karatasi na biki. Vilikua vimelaliwa na mke wangu. Nikawahi nikaiokota ile karatasi na kuiweka mfukoni. Baada ya mda Difenda ikaondoka na miili ile miwili. Walinihitaji pia kituoni nikawaambia watangulie na mimi nitafuata.

Walipoondoka nikaichukua ile karatasi iliyokua na damudamu. Nikaikunjua ndipo nilipokutana na ujumbe mzito wa mke wangu. Ulisomeka hivi. "Mume wangu mpenzi samahani kwa maamuzi niliyochukua, Sikua na namna ya kukwepa aibu hii, ukweli ni kwamba walipotuvamia walianza kumdharirisha mwanetu. Walimlawiti mbele yangu. Walikua wanaume sita wenye unyama uliokubuhu. Baada ya kujiridhisha wakahamia kwangu. Nimebakwa na wanaume sita mbele ya mwanangu na. Nwanangu kalawitiwa mbele yangu. Kisha wakamuua mbele yangu. Sikuona sababu ya kuishi nisamehe. Wanachohitaji ni wewe kuacha uaskari na uache kuwafuatilia hiyo ndiyo salama yako. Naomba nikuachie wosia adui si kumwogopa ni kupambana naye. Naamini unaweza na utawamaliza nakupenda sana na Mungu akipenda tutaonana siku ya uamsho"

Wakati namaliza kusoma ile karatasi nilikua nimedondosha chozi la uchungu. Nililia kilio toka ndani ya moyo. Nilifadhaika haswaa. Nikaona nimepoteza tumaini. Na nilitamani kuwajua wauaji ili niwaue kwa mkono wangu. Potelea mbali jela lakini mke wangu na mwanangu waliniuma sana. Zaidi mwanangu kulawitiwa mbele ya mama yake. Niliapa kulipa kusasi kwa mikono yangu. Hakika hasira kuu iliwaka moyoni mwangu. Nyuma yangu alikuwepo yule mtoto wa marehemu bosi wangu. Nikageuka nikamwona naye analia. Niliumia sana. Nikapigiwa simu ya kua wananingoja kituoni kwenda kutoa amri ya mwisho juu ya miili ile kwani tayari uchunguzi umekwisha.

Nilitoka nje huku uchungu ukiwa umenitawala. Nikakodi taksi nikamchukua yule mtoto tukaenda kituoni. Baada ya kufika nikaulizwa maamuzi yangu. Nikasema atazikwa Njombe. Nikaambiwa ripoti ya uchunguzi nitapewa nikirudi. Walinikabidhi magari kadhaa. Kwakua nilikua sijielewi afande Perisi alisimamia kila kitu. Safari ya kutoka Dar es salaam kuelekea Njombe ikaanza. Nakumbuka Peris ni mtu aliyekua karibu na mimi akinifariji kwa karibu. Alinipenda sana. Nadhani ilikua anaponiona mimi nina tatizo Uafande aliuvua na kuvaa huruma na moyo wa upendo. Nilikua nalia kwa uchumgu njia nzima.

Maaskari wengi sana walinisindikiza. Baada ya kufika Njombe. Tulipumzika siku moja kisha taratibu zikafuatwa mke wangu na mwanangu wakapumzishwa katika nyumba zao za milele. Mungu alitoa, Mungu ametwaa Jina lake libarikiwe. Yalikua ni maneno ya mwisho kutoka kwa mchungaji pale makaburi ni. Nilikua bado siamini kama kweli sitawaona tena katika uso wa dunia. Nilimwaga chozi jicho moja. Nikahisi uaskari mgumu. Lakini kila nilipokumbuka maneno ya mke wangu yalinipa nguvu mpya. "Najua unaweza kuwamaliza...Zzzzzzaaa....Adui siyo kumwogopa ni kupambana....Nnnnaaa.

Hivi ndivyo yalijirudia akilini mwangu yakiwa kama na mwangwi hivi. Ujasiri ukaniingia na kunitawala nikajikuta nachota tena mchanga chini na kuushika kwa nguvu. Machozi yalinitoka Hasira ya kisasi ikachoma na kuunguza nafsi yangu. Nikajisemea moyoni lazima wote waliohusika wafe. Peris akaja kunikumbatia na kunishikilia kama sehemu ya kunisaidia kutembea. Tulirudi nyumbani. Niliomba mapumziko ya kulala kiasi. Nilikua nimezidiwa na mawazo na hasira. Nikapewa mkeka nikajiegesha. Peris hakutoka pembeni yangu alikua akiniangalia kwa ukaribu sana.Mda ukasonga hata usingizi sikupata.

Zilipita siku mbili watu walikua wameshatawanyika wengi. Msibani tulibaki wachache. Hata wale maafande wenzangu walirudi Dar es salaam kuendelea na ujenzi wa taifa. Nilibaki na Peris na Yule mtoto wa bosi wangu. Nikawa kila nikimkumbuka mke wangu nalia. Siku zikasonga hatimaye msiba ukaisha. Kila mtu alitakiwa kurudi kuendelea na majukumu ya kila siku. Hata tungeomboleza miaka mia bado asingerudi. Basi nakumbuka siku naondoka nyumbani babu yangu alinipa baraka na baba na mama pia. Nikatoka Njombe nina hasira na Majambazi na kila anayevunja sheria za nchi. Tulitoka Njombe mimi na Peris ba Anthony yule mtoto wa marehemu bosi. Kichwani nilikua napanga kuua tuu na kuwapoteza wote na sitaacha hata mtu mmoja. Hakika nilikua nimegadhabika. Safari ya kurudi Dar es salaam ikaanza hivo__________________________ ______________________________
_____________________________________________________________________________________________Je afande yuu atafanikiwa kulipa kisasi? Ungana naye sehemu ya 8 tujue yaliyojiri mjini. Kwa lolote niandikie inbox Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Watsap 0755683295. Email@yusuphngahala@,gmail.com na Instagram@mwalim_yuu. Bye bye....
Previous
Next Post »