Watu wanne wamefariki Dunia mkoani mbeya katika matukio mawili tofauti ikiwemo la watu watatu kufariki wafariki baada ya kuangukiwa na kifusi wakiwa katika shughuli za uchimbaji madini.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Ahmed Msangi amewataja waliofariki dunia kuwa ni Victor Sanga (26) mkazi wa mbeya,mwingine amefahamika kwa jina moja la sheta umri kati ya miaka 30-35 na watatu hajafahamika jina wala makazi, jinsi ya kiume, umri kati ya miaka 30-35, wote wachimbaji wadogowadogo wa madini/dhahabu walikutwa wamekufa kwenye shimo lenye urefu wa futi 50 walimokuwa wakichimba dhahabu baada ya kuangukiwa na kifusi.
Amesema tukio hilo limetokea March 11,mwaka huu saa 1:15 jioni huko katika kitongoji cha Mawowo, kijiji cha patamela, wilayani chunya, huku chanzo cha tukio hilo ni baada ya kuta za shimo kuloa maji na kukosa uimara na kisha kuporomoka.
Kamanda Msangi amesema miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya mwambani chunya huku upelelezi zaidi wa tukio hili unaendelea.
Katika hatua nyingine Steward Mandras (55) mkazi wa Uyole amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari lisilofahamika lililokuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika.
Tukio hilo limetokea March 11,mwaka huu saa 1:10 jioni eneo la Sijabaje-Uyole, kata ya igawilo, jiji na mkoa wa mbeya huku chanzo cha ajali kikiendelea kuchunguzwa na dereva alikimbia na gari mara baada ya tukio, jitihada za kumtafuta zinaendelea.
EmoticonEmoticon