Mkazi wa mtaa wa mageuzi kata ya Nsalala Mbalizi Mbeya Tatu Hatibu miaka (40) amelazimika kulala nje ya nyumba yake akiwa na wafamilia yake ya watu 8 baada ya nyumba yake kukumbwa kadhia ya moto wa ajabu. Tukio hilo la ajabu lilianza kutokea alfajiri ya jumatatu wiki hii ambapo moto ulianza kuwaka katika moja ya vyumba wanavyolala watoto ambapo moto huo uliteketeza magodoro wakati watoto wakiwa wamelala.
Jambo la kushangaza katika tukio hilo ni magoro na nguo kuteketea kwa moto huku miili ya binadamu waliokuwa wamelala kwenye magodoro hayo kutopata madhara yoyote. Akielezea mkasa huo Bi Tatu ambaye ni mwathirika wa tukio hilo amesema tukio hilo limekuja siku chache baada ya kushinda kesi dhidi ya jirani yake ambayo iliamriwa katika mahakama ya Mbalizi.
Amesema kesi hiyo ilikuwa inahusu ungomvi wa makazi yeye pamoja jirani yake ambapo katika eneo analo ishi bibi huyo kulikuwa na kipande cha ukuta ambacho kiliongezeka kujengwa hadi eneo la nyumba yake hali ambayo iliibua mgogoro huo. Nao baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ambao ni familia ya Bi.TATU wamesema kutokana na kadhia hiyo hivi sasa wamelazimika kulala nje ya nyumba yao kukwepa maafa zaidi.
Blog hii imeshuhudia familia hiyo ikiwa nje ya nyumba yao kwa kuofiwa kukutwa na maafa zaidi ambapo hadi tunakwenda mitamboni bado moto huo uliendelea kuteketeza baadhi ya vitu katika makazi ya Bibi huyo.. MTU mmoja amepoteza maisha baada ya kupigwa na mtu au watu wasiojulikana na miguuni kwake kukiwa kumefungwa mbuzi aliye hai katika eneo la Nsalala Kata ya Mbalizi Mkoani Mbeya. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Nyagesa Wankyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja marehemu kuwa ni Robart Mwasenga (35) ambaye aliuawa juzi usiku baada ya kupigwa na mtu au watu wasiojulikana kwa tuhuma za wizi.
Inadaiwa kwamba kuwa Marehemu huyo kabla ya kufikwa na mauti alifika kwenye banda la mifugo linalomilikiwa na Wilison Mwangasani ambaye ni jirani yake na kutaka kuiba mbuzi . Ofisa Mtendaji wa Kitongoji cha Nsalala Lwitiko Mwaibindi, amesema alipata taarifa kutoka kwa raia mwema, kwamba kuna mtu anahitaji msaada wa haraka kwani anaonekana amepigwa na kuumizwa.
Amesema badaa ya kuona hali hiyo alilazimika kukimbia hadi kituo cha polisi kwa lengo la kutoa taaraifa hizo majira ya saa 5 usiku ambapo hata hivyo alikuta kituo kimefungwa kwa muda huo.
Amesema baada ya kutumia jitihada binafsi kwa kugonga mlango hatimaye alifunguliwa na mmoja wa askari baada ya dakika 15 tangu afike kituoni hapo na kupokewa kwa kauli za vitisho toka kwa askari huyo ambaye hakuwa tayari kumtaja jina akidai kuwa mwenyekiti huyo amekiuka taratibu kwani muda wa kazi huishia saa 4 usiku hivyo alipaswa kufika asubuhi.
Aidha baada ya askari kumtaka mwenyekiti kurudi kesho yake hali ilibadilika ambapo kulitokea majibizano yaliyopelekea mwenyekiti kuwekwa mahabusu hadi saa 8 mchana siku iliyofuata.
Amesema kitendo cha yeye kuwekwa mahabusu pamoja na askari kushindwa kufika eneo la tukio kwa muda huo kumechangia kwa kiasi kikubwa marehemu kupoteza maisha kwani kulikuwa na uwezekano wa kupona endapo angewahishwa hospitali.
Hata hivyo baada ya sakata hilo kati ya polisi na mwenyekiti, hatimaye mtendaji wa kitongoji alilazimika kufika kituo cha polisi na kumuwekea mzamana mwenyekiti wake majira ya saa 8 chana .
Akijibu tuhuma hizo,Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa mbeya Nyigesa Wankyo amekiri kupokea taarifa hizo na kuahidi kuzifanyia kazi lakini mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zake tayari kwa maziko.
EmoticonEmoticon