MAMLAKA zinazodhibiti ubora wa vyakula nchini,zimetakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kampuni za mawasiliano kwa kutumia fursa ya teknolojia ya mawasiliano ili kuhakikisha kuwa haki za watumiaji wa vyakula zinalindwa na huduma bora zinapatikana.




Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa, akizungumza  wakati akifungua maadhimisho ya Kitaifa ya wiki ya haki za mtumiaji Duniani ambapo kitaifa yanafanyika Mkoani Mbeya katika ukumbi wa mkapa jijini Mbeya





na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA/CCC )


Hawa Ng’umbi
- See more at: http://jamiimoja.blogspot.com/2015/03/habari-picha-uzinduzi-wa-vilabu-vya.html#sthash.67ffRMCW.dpuf
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA/CCC ) Hawa Ng’umbi akizungumza katika  mkutano huo
Wadau na waalikwa katika mkutano huo wakiwa makini kusikiliza mgeni rasmi.











Baadhi ya washiriki wakiwa katika Picha ya pamoja.(Picha na Fahari News)


MAMLAKA zinazodhibiti ubora wa vyakula nchini,zimetakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kampuni za mawasiliano kwa kutumia fursa ya teknolojia ya mawasiliano ili kuhakikisha kuwa haki za watumiaji wa vyakula zinalindwa na huduma bora zinapatikana.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyerembe Munasa, aliyasema hayo jana, wakati akifungua maadhimisho ya Kitaifa ya wiki ya haki za mtumiaji Duniani ambapo kitaifa yanafanyika Mkoani Mbeya, kupitia jukwaa la watumiaji kwa kushirikiana na mamlaka za mawasiliano na mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji wanchi kavu na majini(SUMATRA).

Amesema wafanyabiashara wa vyakula pamoja na kampuni za kuhifadhi, kusindika na kusafirisha vyakula zinatakiwa kuhakikisha kuwa zinatumia fursa zilizopo kulinda na kushajiisha matumizi ya teknolojia za mawasiliano ili kulinda afya za watumiaji.

“Mamlaka zinazodhibiti ubora wa vyakula zinatakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kampuni za mawasialiano kwa kutumia fursa ya teknolojia ya mawasiliano kuhakikisha kuwa haki za mtumiaji wa vyakula zinalindwa na huduma bora zinapatikana,”amesema.

Amesema, kwa kufanya hivyo watakuwa wamehusisha suala zima la kutoa elimu kwa watumiaji kuhusu wajibu na haki zao na kutoa tahadhari kwa watumiaji endapo bidhaa zisizokidhi vigezo vya kuwepo sokoni zinapati
Previous
Next Post »