Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
Mosi Mei, 2017 amesema Serikali ya Awamu ya tano imepanga kufanya
nyongeza ya kawaida ya kila mwaka katika mishahara yaani Annual
increment, ambayo ilikuwa imesimama kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na
promosheni.
Rais
Magufuli ametoa ahadi hiyo katika Sherehe za siku ya Wafanyakazi
duniani zilizofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoani
Kilimanjaro.
Amesema
uamuzi wa Serikali wa kuanza kutoa promosheni unatokana na kukamilika
kwa zoezi la uhakiki wa Wafanyakazi hewa zaidi ya wafanyakzi kumi
19,000 walibainika kuwa wafanyakazi hewa.
''Yale
mambo yote yaliyokuwa pending ikiwa ni pamoja na promosheni kwa sababu
tulishindwa, unaweza kupromoti mfanyakazi hewa hayupo,kwa sababu
tungetoa promosheni wakati kuna wafanyakazi 19,000 hewa,maanake
tungepromoti na 19,000 na siajabu na watu waliowaandika mule ndio
wangeletwa katika mapendkezo ya promosheni'' amesema Rais Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli amewaonya watumishi ambao wamekuwa wakidanganya umri wa
kustaafu ili waendelee kufanya kazi kwa muda mrefu na kuwa siku zao sasa
zimekwisha.
Katika
hatua nyingine Rais Magufuli amepiga marufuku uhamisho wa Wafanyakazi
bila kuwalipa stahili zao kutokana na kuwepo na tabia ya kuwahamisha
wafanyakazi bila kuzingatia taratibu hasa za malipo ya uhamisho.
''Sasa
niwaombe wafanyakazi yeyote akihamishwa hakuna kuhama mpaka umelipwa
pesa ya uhamisho,kuanzia juu mpaka chini,yeyote atakaye kuhamisha
mwambie nipe hela yangu ya uhamisho ninapoenda akishindwa usihame kaa
hapohapo ufanye kazi'' Amesema Rais Magufuli.
Amesema
viongozi wengine wamekuwa wakiwahamisha wafanyakazi kwa maslahi
binafsi au visasi kutokana na maendeleo wanayowapata wafanyakzi
Rais
Mgufuli amewahakikishia wafanyakazi kuwa Serikali ya awamu ya Tano
itaendelea kuwajali na kuwa karibu nao katika kutimiza dhana ya utatu
ya ushirikiano kati ya Serikali, Wafanyakazi na Waajiri kwa lengo la
kuleta maendeleo.
Aidha,
Rais Magufuli amewaeleza wafanyakazi mipango mbalimbali anayofanywa na
Serikali katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege
mpya ,ujenzi wa Reli ya kisasa, utoaji elimu bila malipo na uboreshaji
wa miundombinu katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Sherehe
za Mei Mosi zilizofanyika katika mkoa wa Kilimanjaro pia zimehudhuriwa
na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Mawaziri, Manaibu Mawaziri,
Wabunge na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali ambapo kauli mbiu
inasema,'' Uchumi wa Viwanda uzingatie kulinda Haki, Maslahi na Heshima
ya Mfanyakazi''.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Moshi, Kilimanjaro
1 Mei, 2017
EmoticonEmoticon