TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 06.05.2015.
·
MAJAMBAZI WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI MKOANI MBEYA KWA KOSA LA KUVAMIA NA KUPORA MALI.
·
WATU SITA WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI KUACHA
NJIA NA KUPINDUKA MKAONI MBEYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
WAWILI WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAKIWA NA SILAHA AINA YA SHOT GUN
ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI IKIWA NA RISASI NNE [04] BAADA YA KUVAMIA NYUMBANI KWA
SUNILDUTT CHARIE (45) MHINDI, MHASIBU
WA SHIRIKA LA KILIMO CHA MPUNGA “KAPUNGA
ESTATE” WILAYANI MBARALI NA
KUPORA PESA TASLIMU NA MALI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 05.05.2015 MAJIRA YA SAA
07:30 ASUBUHI HUKO KWENYE SHIRIKA LA KILIMO CHA MPUNGA KAPUNGA ESTATE, KIJIJI CHA KAPUNGA, KATA YA MAPOGORO, TARAFA YA
ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
MAJAMBAZI HAYO YALIFIKA NYUMBANI KWA MHANGA NA KISHA
KUJITAMBULISHA KUWA NI WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA KILIMO CHA MPUNGA “KAPUNGA ESTATE” NA NDIPO WALIMVAMIA
MHANGA NA KISHA KUMPORA PESA TSHS 320,000/=,
USD 275, INDIAN RUPIA 2,000 NA
SIMU MBILI ZA MKONONI AINA YA TECNO.
WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA MALI ZOTE WALIZOPORA PAMOJA
NA SILAHA. MHANGA AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
WATU SITA WAJERUHIWA BAADA YA BASI WALILOKUWA
WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.844
AZR AINA YA NISSAN MALI YA KAMPUNI YA MBEYA EXPRESS LILILOKUWA LIKIENDESHWA
NA DEREVA AITWAYE EMANUEL MWASHAMBWA
LIKITOKEA MBEYA KWENDA MWANZA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA KATIKA KIJIJI CHA
SHAMWENGO NJE KIDOGO YA JIJI LA MBEYA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 05.05.2015 MAJIRA YA SAA
14:13 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHAMWENGO, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI,
KATIKA BARABARA YA MBEYA/IRINGA.
MAJERUHI KATIKA AJALI HIYO NI 1. GODWIN SIMULUNGA (47) MKAZI WA IYUNGA JIJINI MBEYA 2. LEGUSY MICHAEL (48) MKAZI WA IYUNGA
JIJINI MBEYA 3. EDSONI MTAFYA (30)
MKAZI WA TUKUYU 4. KATABARO FREDY (22)
MKAZI WA SINDE 5. CHARLES MWAKABENGA
(24) MKAZI WA UYOLE NA 6. NOVELI
ASHAM (27) MKAZI WA TUKUYU. MAJERUHI WOTE WAMETIBIWA KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA NA KURUHUSIWA.
DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI, JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUFUATA SHERIA/KANUNI NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[NYIGESA R.
WANKYO – ACP]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon