·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE WAWILI
KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUPINDUKA.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI WAKIWA NA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
GARI LENYE NAMBA
ZA USAJILI T.959 BMM AINA YA TOYOTA
L/CRUISER 110 LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA FARAHAD ABDUL (26)
MWARABU – MSIMAMIZI WA KAMPUNI YA KUCHENGUA DHAHABU YA PIRBAKISH MKAZI WA
CHUNYA LILIPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA SEIF
MOHAMED (27) MKAZI WA NZEGA.
AJALI HIYO
IMETOKEA MNAMO TAREHE 27.04.2014
MAJIRA YA SAA 22:45 USIKU HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, BARABARA
YA MAKONGOLOSI/MKWAJUNI, WILAYA YA CHUNYA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WAWILI
WALIJERUHIWA 1. FARAHAD ABDUL (26)
DEREVA WA GARI HILO AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA RAYMOND SIKAONA (29) MFANYAKAZI KATIKA HALMASHAURI YA MJI MDOGO WA MAKONGOLOSI
AMBAYE ALIKUWA ABIRIA NA AMELAZWA HOSPITALI YA
MWAMBANI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA JAPO
KUWA AMELAZWA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA
NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
KATIKA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA
KWANZA ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA SANGAMBI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA MTU MMOJA AITWAE JAPHET NZOWA (39) MFANYABIASHARA, MKAZI
WA SANGAMBI AKIWA NA POMBE KALI[VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA
YA BOSS
PAKETI 173 NA RIDDER PAKETI 60.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 28.04.2014
MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA
PILI ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHOGA, KATA YA SANGAMBI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA JOHN DAWILO (29) MKAZI
WA SHOGA AKIWA NA POMBE KALI[VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA
YA BOSS
PAKETI 61 NA RIDDER PAKETI 15.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 28.04.2014
MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:-
[AHMED Z. MSANGI
– SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon