TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 12.03.2015.
·
WATU WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA
NA KIFUSI WAKIWA KATIKA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA
BARABARANI JIJINI MBEYA.
·
WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA WAKIWA NA KETE ZA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. VICTOR
SANGA (26) MKAZI WA MBEYA 2. AMEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA SHETA UMRI KATI YA MIAKA 30-35 NA 3. HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI, JINSI
YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 30-35, WOTE WACHIMBAJI WADOGOWADOGO WA
MADINI/DHAHABU WALIKUTWA WAMEKUFA KWENYE
SHIMO LENYE UREFU WA FUTI 50 WALIMOKUWA WAKICHIMBA DHAHABU BAADA YA KUANGUKIWA
NA KIFUSI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.03.2015 MAJIRA YA SAA
19:15 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAWOWO, KIJIJI CHA PATAMELA, KATA YA
SAZA, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO
TUKIO HILO NI BAADA YA KUTA ZA SHIMO KULOA MAJI NA KUKOSA UIMARA NA KISHA
KUPOROMOKA.
MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MWAMBANI
CHUNYA. UPELELEZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA STEWARD MANDRAS (55) MKAZI WA UYOLE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA
GARI LISILOFAHAMIKA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.03.2015 MAJIRA YA SAA
19:10 JIONI HUKO ENEO LA SIJABAJE-UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA
TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
TAARIFA ZA MISAKO:
WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. DIAMUND MANYERERE (24) MKAZI WA MOPOROMOKO NA 2. REMSI BUNGE (20) MKAZI WA MAKAMBINI
WILAYANI MOMBA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI KETE 03 SAWA NA UZITO WA GRAM 15.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 11.03.2015 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MSITU WA
IDARA YA MAJI, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA WACHIMBAJI MADINI KUWA MAKINI HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA
ZINAZOENDELEA KUNYESHA KWA KUCHUKUA TAHADHARI ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA
ALIYESABABISHA KIFO NA KISHA KUKIMBIA AZITOE ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon