WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 18 KUJERUHIWA WAKITWA KATIKA HARAKATI ZA KUIBA MAFUTA WILAYA YA RUNGWE.




TAARIFA YA  JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 19.02.2015.

Ø  WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 18 KUJERUHIWA WAKITWA KATIKA HARAKATI ZA KUIBA MAFUTA  WILAYA YA RUNGWE.

Ø  MTUHUMIWA MMOJA AKAMATWA NA BHANGI WILAYA YA MBEYA.
 
Ø  MTUHUMIWA MMOJA  AKAMATWA NA MAFUTA AINA YA DIESEL YANAYODHANIWA KUWA YA ZIZI  WILAYA YA MBEYA.
 

TUKIO LA KWANZA.

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 18 KUJERUHIWA WAKITWA KATIKA HARAKATI ZA KUIBA MAFUTA  WILAYA YA RUNGWE.


WATU WAWILI 1. MARIA PAJELA [18] NA 2. WILLIAM S/O PASCHAL [38] ,WOTE WAKAZI WA KIJIJI  CHA IDWELI,WALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUUNGUA MOTO KIJIJINI HAPO.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE  18.02.2015 SAA 21:00HRS KATIKA KIJIJI CHA IDWELI, KATA YA ISONGOLE,  TARAFA YA UKUKWE.

KATIKA TUKIO HILO MAREHEMU HAO PAMOJA NA BAADHI  YA WANANCHI WENGINE WA KIJIJI HICHO WALIKUWA KATIKA HARAKATI ZA KUIBA MAFUTA KUTOKA KATIKA GARI T.891 AQZ /T.821 ARF AINA YA SCANIA MALI YA AILIS SANGA LILILOKUWA LIMEBEBA MAFUTA AINA YA PETROLI UJAZO WA LITA 41,000, LIKITOKEA DSM KUELEKEA NCHINI MALAWI,  LIKIENDESHWA NA DEREVA ZAWADI NYATO [46] MKAZI WA SAE MBEYA AKIWA NA TINGO WAKE FRANK YOHANA [24],MKAZI WA MBOZI.

AWALI KABLA YA TUKIO HILO GARI HILO LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA, HIVYO WAHANGA [DEREVA NA TINGO] WALIFANIKIWA KUOKOLEWA NA KUPELEKWA KITUO CHA POLISI KIWIRA ILI KUPATA HATI YA MATIBABU [PF3] KWA AJILI YA KWENDA HOSPITALINI KUPATIWA MATIBABU. HATA HIVYO BAADHI YA WANANCHI WA ENEO HILO WALIVAMIA GARI HILO NA KUFANIKIWA KUTOBOA TANKI LA MAFUTA, HALI ILIYOPELEKEA MAFUTA KUANZA KUMWAGIKA/KUSAMBAA MAENEO HAYO NA HATA KUELEKEA MAENEO YENYE MAKAZI YA WATU  NA WAO KUKINGA KWA KUTUMIA VYOMBO VYAO.


KATIKA TUKIO HILO WATU KUMI NA NANE [18] WALIJERUHIWA, KATI YAO WANAUME NI 13 NA WANAWAKE 05 AMBAO NI: 1. SHUKURU KANZALE [21], 2. NURU GEORGE [30], 3.ASANTE BONIFACE [38], 4. JOSEPH JAMSON [18], 5.JOSEPH PASCHAL [30], 6.SIZA KANESA [22], 7.ALEX  DAUD [35], 8. OSCAR YOSIA [23], 9.TRAIPHON MOASI [37], 10.SAMSON MBWILA [29].

WENGINE NI 11. DORA MICHAEL [35],12. VERONICA ELIA [30],13.RABSEN AYUB [26], 14.WASIWASI SPIKA [32], 15.ASIA ANON [20], 16.BAHATI KYANDO [23], 17. CHRISTOPHER ERASTO [32] NA 18. MELISA SANANE [50], WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IDWELI. AIDHA KATI YA MAJERUHI HAO,MAJERUHI 16 WAMELAZWA HOSPITALI YA MISHENI –IGOGWE NA MAJERUHI WAWILI WAMELAZWA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA-TUKUYU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.











MISAKO:

WATUHUMIWA WAWILI WAKAMATWA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI   WILAYA YA MBEYA.

TUKIO LA KWANZA.

KATIKA TUKIO LA KWANZA YONA MWANJELA [42] MKAZI WA SIMIKE-MBEYA, ALIKAMATWA AKIWA NA MAFUTA AINA YA DIESEL UJAZO WA LITA 1,100 MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI.


TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 18.02.2015 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA EENO LA SIMIKE, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA JIJINI MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.

TUKIO LA PILI.

KATIKA TUKIO LA PILI  SOMON NICHO  [32] MKAZI WA KALOBE – MBEYA ALIKAMATWA AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 100.

TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 18.02.2015 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA ISYESYE, KATA YA ISYESYE,TARAFA YA IYUNGA,JIJINI MBEYA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANATOA  WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI KUHUSIANA NA MAJANGA YA MOTO.


AIDHA KAMANDA MSANGI ANAENDELEA KUTOA  WITO  KWA WANANCHI  HUSUSANI WAKAZI WA MKOA WA MBEYA   KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI INA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII IKIWA NI PAMOJA NA KUPOTEZA UHAI NA NGUVU KAZI YA TAIFA, BADALA YAKE WAHESHIMU NA KUTII MAMLAKA ZILIZOWEKWA KWA MUJIBU WA SHERIA NA SHERIA ZA NCHI KWA UJUMLA.



[ AHMED  Z. MSANGI – SACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



Previous
Next Post »