BAADHI YA PICHA ZILIZOKO KWENYE VIPANDE VYA FILAMU YA VANILA.
Na Mwandishi wetu,Mbeya.
WADAU wa sanaa ndani na nje ya mkoa wa Mbeya
wameombwa kutoa ushirikiano kwa wasanii wa filamu mkoani hapa kwa kununua kazi
zinazofanywa na kuacha kasumba kuwa filamu bora zinaweza kutengenezwa na
wasanii walioko Dra es salaam pekee.
Mwongozaji wa filamu wa kampuni ya Pritauj Filim
Prince Hekela alitoa rai hiyo jana alipokuwa akitambulisha Filamu mpya ya
Vanilla iliyochezwa na wasanii kutoka mkoani Mbeya.
Prince Hekela alisema kumekuwa na kasumba ya baadhi
ya wadau kuamini filamu nzuri ni zile zinazochezwa na wasanii wa Dar es salaam
jambo alilosema limekuwa likididimiza sana wasanii wa mikoani.
Alisema ni wakati kwa wadau hao kutambua kuwa ubora
wa filamu hautokanani na mahali anakofanyia kazi zake msanii,bali umakini na
maandalizo bora ndiyo msingi wa kutengenezwa kwa filamu bora.
Akizungumzia filamu ya Vanila aliyosema tayari
imeingizwa sokoni,alisema imeandaliwa katika mazingira yenye kuzingatia staha
hivyo haina vipande vyenye kuonesha aibu kiasi cha familia kushindwa kuitazama
kwa pamoja.
“Vanilla ni filamu ambayo hata ukienda kuonesha
uwanjani hakuna kinachozuia.Kwa nyumbani hata awepo baba mama na watoto
wanaweza kuiangalia kwa pamoja.Na ina mafundisho ya kila mtu kulinagana na umri
wake”
“Muhimu pia wadau watambue kuwa tumejipanga
kuhakikisha tunaleta burudani nzuri kutokana na filamu zetu.Ndiyo sababu hata
katika Vanila utaona tumechanganya wasanii wapya na wa zamani.Wasanii wapya
ambao wamefanya vizuri sana katika filamu hii ni pamoja na Issa Ngoda,Regina
Mwinyi, Kelvin Kaziyandege na Joachim Nyambo.Lakini pia tumemshirikisha
mwanadada Riyama Ally ambaye ni mkongwe katika sanaa” alisisitiza Hekela.
Kwa upande wake mmoja wa wasanii waliocheza filamu
ya Vanila Joachim Nyambo alisisitiza kuwa filamu hiyo imekuja kuwadhihirishia
wadau kuwa kazi nzuri ya sanaa inaweza pia kufanyika mikoani.
Nyambo aliwasihi wadau kuendelea kushirikiana na
wasanii mikoani wanaoonekana kukuza sanaa kwa kuwa michango ya hali na mali ili
kuwezesha kukua kwa sanaa.
Mwisho.
EmoticonEmoticon