TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 26.01.2015.
·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUCHOMWA KISU WILAYA CHUNYA.
·
MTOTO WA MIAKA 04 AFARIKI DUNIA BAADA YA
KUGONGWA NA PIKIPIKI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WATU WAWILI WAKIWA NA MALI ZINAZODHANIWA NI ZA WIZI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AKIWA NA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA
MTU MMOJA AITWAYE GODUELO
ZUMBA (45) MKAZI WA KIJIJI CHA IFWENKENYA WILAYANI CHUNYA AKIWA NYUMBANI
KWAKE ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI NA UBAVUNI UPANDE WA KUSHOTO NA MTU
MMOJA AITWAYE MAMBWE MWANALELE (35)
MKAZI WA KIJIJI CHA IFWENKENYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 25.01.2015 MAJIRA YA SAA
20:30 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA IFWENKENYA, TARAFA YA SONGWE,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO NI WIVU WA KIMAPENZI
BAADA YA MTUHUMIWA KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MPENZI
WAKE. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA PILI
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 04 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FREDY CHANGULA MKAZI WA ILOMBA ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA
KUFIKISHWA HOSPITALI YA MKOA KWA AJILI YA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA
PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.525
CXF AINA YA KINGLION ILIYOKUWA IKIENDESHWA
NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 25.01.2015 MAJIRA YA SAA
10:00 ASUBUHI HUKO ENEO LA ILOMBA, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI
NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA, JITIHADA ZA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ZINAENDELEA BAADA YA KUKIMBIA
MARA BAADA YA AJALI HIYO.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.
EMANUEL DAUD (19) NA 2. SIYAWEZI YOHANA (23) WOTE WAKAZI WA
MTAA WA MWAKA WAKIWA NA REDIO 3 AINA YA
PIONEER, PHILIPS NA RISING, DECK YA TV MOJA, NYANYA ZA REDIO ZA AINA MBALIMBALI PAMOJA NA SIMU YA MKONONI AINA YA TECNO MOJA.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO
MNAMO TAREHE 25.01.2015 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO KATIKA MTAA WA
SIKANYIKA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU
ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA AITWAYE IBRAHIM HAHOBOKILE
(25) MKAZI WA MTAA WA UYOLE AKIWA NA BHANGI KETE SABA [07] SAWA NA UZITO WA GRAM
35.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 25.01.2015 MAJIRA YA SAA 15:40 JIONI HUKO KATIKA MTAA WA NSALAGA-UYOLE,
KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA
MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
Imesainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
EmoticonEmoticon