JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 21 RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 28.01.2015.

JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 21 RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI.

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA  NDAIZABA SELEPIN (25) NA WENZAKE KUMI NA TANO [15], KATI YAO WATU WAZIMA 08 NA WATOTO 08, WOTE NI RAIA NA  WAKAZI WA NCHINI BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.01.2015 MAJIRA YA SAA 04:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANDETE, KATA YA ITOPE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.

AIDHA KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA NA WAKAZI WATANO WA NCHINI BURUNDI WALIFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.  ABEL TUGIMANA (23) 2. BARANDA GODFREY (25) 3. SENGIUMVI GABRIEL (14) 4. DUAYO BOSCO (20) NA 5. NIMAYE SIPELANSA (25) WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 27.01.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA ISANGA, KATA YA ISANGA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WAGENI KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA KISHERIA WANAPOTAKA KUINGIA NCHINI ILI KUEPUKA MATATIZO. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

                                                         
                                                       Imesainiwa na:
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA MBEYA.
 


Previous
Next Post »