WEKUNDU
wa Msimbazi Simba wamekubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Wagonga
Nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara
iliyomalizika jioni hii uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mabao
ya Mbeya City yamefungwa na Hamad Kibopile na Yusuph Abdallah aliyefunga kwa
njia ya penalti, wakati la Simba limefungwa na Ibrahim Hajib ‘Mido’.
Hata
hivyo dakika ya mwisho ya mchezo, Masoud Nassor ‘Cholo’ amekosa mkwaju wa
penalti baada ya beki Yusuph kumfanyia madhambi Jonas Mkude katika eneo la
hatari.
Hiki
ni kipigo cha pili kwa Simba ndani ya uwanja wa Taifa, kwani desemba 26 mwaka
jana walifungwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.
EmoticonEmoticon