MSIMULIJI.SAIMENI MGALULA
Michael oga alikuwa ni mfalme katika jimbo la Swai huko Tanzania pamoja na kuwa mfalme lakini alikuwa anawanyanyasa sana maskini kitu kilicho pelekea anakuja kupata lana kutoka bibi kizee ambaye alikuwa ombaomba anatoa maneno kwa makali kwa mfalme na hatimaye anapata lana songa sasa na mm iliuone ni lana gani alipata mfalme huyo.
NI bibi mmoja mbaye alikuwa anaishi maisha ya kuomba omba msaada wa chakula katika jimbo la swai ,anakuja kukutana na Warembo wawili anawaomba msaada wanamuangalia tu ghafla anatokea mama mmoja ambaye alikuwa na kichanga mgongoni anatoa shilling mia mbili na kuweka katika mikono yake.
Wakati bibi huyo akiendelea kujikongoja na mkongoji wake akiwa kando kando ya barabara kwa mbele yake kulikuwa na gari ndogo ambayo ilikuwa imeharibika ya mtu baki ndipo punde si punde unatokea msafara wa mfalme oga unasimama na wanashuka wale wafuasi wake na kuanza kumpiga Yule mtu ambaye alikuwa amepaki gari barabarani na kuisukuma gari lake pembeni.
Mara baada ya tukio hilo anashuka mfalme oga na kuwauliza wafuasi wake kuwa kuna nini hapa kabla haja maliza anakutamikono michafu ikimgusa kwenye miguu yake pamoja na nguo zake na harufu kali ambayo ilitoka kumbe alikuwa ni Yule bibi akitaka msaada kutoka kwa mfalme oga na msaada wake ulikuwa ni chakula tu si kitu kingine .
Lakini cha kushangaza mfalme oga anawahamuru wafuasi wake kumtoa Yule bibi na kumpiga kumbe Yule bibi kile kitu kimemkera sana ndipo alitamka maneno yaha alisema umeninyanyasa sana na kuniita mbaya pia mchafu sasa wewe ndio utakuwa mbaya zaidi yangu mpaka utakapo anza kuwasaidia maskini na kuwajari lakini mfalme anaona poa na kuanza kunusa nguo ambazo aliguswa na Yule bibi nakutaka abadirishwe palepale.
Ghafla wafuasi wanachukuwa nguo kubwa na kuzungushia eneo ambalo alikuwa amesimama mfaslme na kubadilisha zingine kasha anaingia ndani ya gari na kuendelea na safari ,Yule mtu ambaye alikuwa amepigwa kisa kuweka gari barabarani aneenda kumsaidia Yule bibi na kumuokotea mkongiji wake ili aendelee na safari kwani gari yake lilikuwa bovu.
EmoticonEmoticon