MSIMULIAJI. SAIMENI MGALULA
Wakati huo sehemu ya pili tunamuona msichana mmoja mrembo SWAUMU CHACHA ambaye alikuwa anaishi katika familia ya kimaskini sana anakuja kutokea mwanaume ambaye alikuwa anapesa nyingi sana lakini kutokana na dharau zake alizonazo kwa wazazi wa binti je atafanikiwa.ENDELEA CHINI HAPA
Ilipoishia Swaumu Chacha kutokana na uzuri wake aliopewa na mungu kumjaharia kuwa na ngozi nyeupe pia ni ya asili lakini anatokea katika familia ya kimaskini ambayo ilikuwa na kijumba kibaya cha nyasi ambacho kilikuwa hakina kitu ndani hata kimoja.
Ndipo anatokea mwanaume mmoja aliye kuwa anaitwa Cash money jina hilo alipewa na wazazi wake pindi alipokuwa mdogo kutokana na bahati alizokuwanazo cash ,lakini Cash anaamua kwenda kwa wazazi wa mwanadada Mrembo Swaumu Chacha ambapo alivyo fika alimkuta mzazi wa mwanamke ndipo alianza kumwambia kuwa wewe mama mwambie mwanao anikubalie mimi nitawajengea nyumba nzuri ya kifahari na kuwanunulia kila kitu vitakuwemo ndani ya nyumba hiyo.
Pamoja na kufanya hivyo kumbuka kuwa alikuwa ajatumia busara yeyote kabla ya mama kumjibu ghafla akatokea binti yake Swaumu mama kwa kutumia akili akamuacha nje kijana Cash iliwakutane na binti yake na aliamua kufanya hivyo ni kwasababu yeye anamjua mwanae kuwa ni mtu mwenye akili nyingi sana za kufikiria kwani alikuwa ni mrembo aliye kuwa ametulia sana pale kijijini kwao na watu alimpenda kutokana na tabia yake.
Cash bila kujari nini?alianza tu na kusema wewe Swaumu mimi nataka kukuoa wewe na ukinikubalia kitayabadilisha maisha yenu mtakuwa na maisha yalio bora kuliko haya,mrembo Swaumu alimjibu kuwa nani?anataka maisha mazuri kama hayo na ni nani ?aliyemwambia kuwa wao ni maskini kitu alicho mjibu ni hikihapa alimwabia kuwa kama yeye anampenda basi anze kujenga nyumba kwanza na kuwanunulia vitu hivyo sio kuongea kwa maneno kama wanaume wa leo wanavyo wadanganya wanawake.
Wakati huo tunaenda kuona mfalme akiwanarudi kwake ambapo alikuwa anaishi kabla ya kuingia ndani mfwasi wake mmoja anatandika mkeka iliapita aliposhuka chini tukutoka kwenye gari lake anawaona watu wawili ambao waliambiwa waje kwa mfalme waeleze shida zao ndipo wapewe msaada wowota lakini chakushangaza mfame oga aliwafukuza kama mbwa kiasi kwamba hata wewe binadamu unayesoma huwezi kufanya hivyo.
Basi sababu yeye ndo mfalme Oga alikuwa yeye ni yeye aliingia ndani na kwenda kukaa kwenye kiti chake ambacho huwa anapumzikia ndipo wakaja wadada watatu ambao kazi yao ilikuwa ni kumpetipeti mfalme oga iliawe anadeka kama mototo mdogo si unajua tena ukiwa na Warembo tena.
Wale wadada watatu walimvua sendoa alizokuwa amevaa miguuni na cheni ambazo alikuwa amevaa shingoni na kumaliziwa na vidani alivyovaa mikononi walivyo maliza kumvua walimnawisha kwa maji ya moto huku wakimuandalia chakula kwaajili ya kula .
GHAFLA MAMBO YANA BADILIKA KWA MFALME OGA
Wakati wadada wazuri wakiendelea na maandarizi ya chakula huku wakiwa wamemuacha mfalme kwenye kile chumba ambacho huwa anapumzika marabaada ya kumaliza kuandaa mmoja aliambiwa aende kumwita wasijue mfalme oga kimemkuta nini?
Kumbe yale maneno aliyo ambiwa na Yule bibi yametimia alibadilika ghafla na kuwa mwenye umbo la sokwe kucha ndefu na kuota manyoya mwili wake wote kama mnyama wa porini na si binadamu wa wakawaida sababu alibadilisha mpaka sauti ikawa kama ya samba dume pori lana iyo ilivyo mkuta wewe hata yeye hakuamini kitu kilivyo mtokea mpaka amekuwa vile .
Baada ya kumkuta ya kumkuta Yule mdada alivyo ingia tu kuona vile alipiga kelele eeeeeeeeeeeeee!jamani kimemkuta nini mfalme huuuuuuuuuuuuuuuuuuuu! mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm mamamaaaaaaaaaaaa!na kukimbia hadi kwa wenzake na kuwaambia .
Yeye baada ya kuona hivyo alichukua kioo ajiangalia kiuwa je sura imebadilika au imekuwaje mbona alivunja kioo na kuanza kupiga kelele kutokana na alivyokuwa amepewa lana ,Ndipo aliwaambia vijana wake watatu waende kule kwa Yule bibi wakamchukue haraka je walivyo enda walimkuta Yule bibi maeneo yale na tukaona kuwa Cash na upendo wake ataendelea kufanikiwa endelea kufatilia uhondo huu mtamu wenye mafunzo mengi itaendelea kesho.0758371860,au0719396851 kama unaushauri ni shauri kwa sms
EmoticonEmoticon