Mtanzania ateuliwa kuwa Makamu wa rais wa mitandao ya BET


Tanzania imepata nafasi kubwa katika shirika la habari za burudani BET lililoko chini ya kampuni ya Viacom Inc, baada ya mtanzania Kay Madati kuteuliwa na kampuni hiyo kuwa makamu mkuu wa rais (Executive  Vice President) na pia Chief Digital Officer.
Kufuatia uteuzi huo, Madati atakuwa na kazi ya kuziongoza timu zote za BET kwenye mitandao ya kijamii na mitandao mingine inayounganishwa na BET.com (BET Networks), pia katika uzalishaji wa vipindi na uendeshaji wa teknolojia na bidhaa.
“We are thrilled to welcome Kay to the team, and look forward to his expertise and strategic leadership in the fast-paced world of digital and social media, as consumers continue to turn to BET to discover what is hot and what is next.” Alisema Mwenyekiti mtendaji wa BET, Debra L. Lee.
Madati atakuwa chini ya mwenyekiti huyo mtendaji wa BET.
Previous
Next Post »