Iran: Wafungwa miaka sita na bakora 91 kwa kucheza wimbo wa Pharrell 'Happy' (Video)


Kundi la wasichana na wavulana sita wa Iran waliocheza wimbo wa Pharrell Williams ‘Happy’ na kisha video yao kusambaa kwenye mitandao mwezi May mwaka huu wamekamatwa tena rasmi na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela na bakora 91.
Hukumu hiyo inakuja ikiwa ni miezi kadhaa tangu walipokamatwa kwa kosa hilo na kuachiwa kwa muda baada ya watu mbalimbali duniani kukemea kwa nguvu kitendo hicho kwa kuwa waliamini vijana hao walikuwa wanajifurahisha tu.
Hata hivyo, kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa kinyume na sheria za nchi hiyo hususani mavazi waliyokuwa wamevaa na aina ya michezo waliyoicheza.
Vijana hao walikiri kosa hilo na kueleza kuwa walirubuniwa na watu kuwa ilikuwa sehemu ya usaili wa kazi ya uigizaji jijini Tehran.
Muda mfupi baada ya hukumu hiyo kutajwa, mwanasheria wa aliyekuwa anawatetea vijana hao, Farshid Rofugaran ameeleza kuwa hukumu hiyo imesamehewa kwa mujibu wa sheria na kwamba itatekelezwa endapo vijana hao watarudia kosa kama hilo ndani ya kipindi cha miaka mitatu.
Previous
Next Post »