WATANZANIA WAMETAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI BORA KATIKA CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA MBOZI

Na Saimeni Mgalula,Mbeya

Watanzania wametakiwa kuchagua viongozi wanao faa na wenye kupenda maendeleo katika jamii pasipo kuangalia sura wala wasifu wa mtu katika chaguzi zijazo.

Hayo yalisemwa jana na Dr Moses Mgara katka mkutano wa hadhara wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) uliofanyika katika viwanja vya Isansya Wilayani Mbozi Mkoani hapa,alisema maendeo mengi yanashindwa kukamilika kwa wakati kutokana na Watanzania kuwachagua Viongozi wasiokuwa na mapenzi bora na Wananchi wao bali wanakuwa na hutu na madaraka.

Dr mgara aliendelea kwa kusema kuwa Desemba mwaka huu kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za mitaa hivyomuafaka wa Watanzania kuchagua Viongozi wanaofaa kwa kuongoza kwa miaka mitano na wapenda maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa chama cha walemavu Wilayani mbozi ambaye pia ni katibu wa Baraza la Wanawake Chadema  Amina Solar amewasihi Wanawake kujitokeza kwa wingi ilikuwania nafasi za Uongozi ili kuleta mabadiliko katika jamii husika

Pia alisema kuwa kumekuwa na changamoto nyingi zinazowakabili katika jamii na ambazo hazijafanyiwa ufumbuzi kutokana na uchache wa wanawake wanaojitokeza kuwania nafasi za uongozi ,hivyo kuwasihi kujitokeza kwa wingi ili kuwania uongozi na kuleta mabadiliko.

Akimalizia Mkazi wa Kijiji cha Isansya Acksoni Ryanda aliwasihi viongozi watakao Chaguliwa kutekeleza ahadi zao za maendeleo kwa muda muafaka na si kusubiri kipindi cha uchaguzi na si wananchi kuishi maisha ya shida.

MWISHO.
Previous
Next Post »