Waziri mkuu Mizengo Pinda azitaka halmashauri nchini kuingiza teknohama kwenye mifumo yao ya ukusanyaji mapato.

Waziri mkuu Mizengo Pinda amezitaka halmashauri zote nchini kuingiza teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) katika mifumo yake ya ukusanyaji wa mapato ili kuepusha misuguano na wananchi wakati wa ukusanyaji wa ushuru na  kuinua kipato cha halmashauri.
Waziri mkuu Mizengo Pinda ametoa wito huo wakati akizindua kituo kipya cha mabasi ambacho kimejengwa na halmashauri ya jiji la Mbeya kwa ufadhili wa benki ya dunia katika eneo la nanenane jijini Mbeya.
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amesema kukamilika kwa mradi huo jijini Mbeya ni matokeo mazuri ya ushirikiano baina ya watendaji na wanasiasa.
 
Kwa upande wake meya wa jiji la Mbeya, Athanas Kapunga amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanaopotosha ukweli juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa kuuhusisha siasa za sasa, huku mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Mussa Zungiza akielezea manufaa wanayoyapata wananchi yanayotokana na kukamilika kwa mradi huo.
 
Previous
Next Post »