AY amepata nafasi ya kuingia ikulu ya Marekani kupitia mualiko maalum wa rais Obama kwa wasanii wa Afrika ambao walikuwa katika One Campaign yenye lengo la kuhamasisha kilimo Afrika.
AY ameungana na wasanii wengine wa Afrika akiwemo Femi Kuti, D’Banj, Fally Ipupa, Victoria Kimani na Owamuni.
Waimbaji hao wanaungana na mchezaji wa Manchester City, Yaya Toure jijini Washington D.C, mkutano ambao umeanza August 4 na utakamilika August 7.
Kikao hicho kitahudhuriwa na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali ya Marekani pamoja na wajumbe wa Young African Leaders Initiative (YALI).
Angalia picha zaidi:
Ay na D'Banj
EmoticonEmoticon