Jay Z na Beyonce wanaendelea na ‘On The Run Tour’ ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.
Taarifa za maandilizi ya talaka kati ya wanandoa Jay Z na Beyonce zimendelea kuandikwa na vyombo vikubwa vya habari ambavyo huaminika sana nchini Marekani na Uingereza.
Taarifa hizo zinazotolewa na vyanzo vya karibu zinaeleza kuwa wanandoa hao wameshatengana hata vyumba vya kulala wakati wakiwa wanaendelea na tour yao.
Hata hivyo, Beyonce amekuwa kimya huku akitumia lugha ya picha mara kadhaa kueleza kinachoendelea, na hivi sasa ameamua kutumia kucha zake kuonesha jinsi yeye na mumewe walivyoshibana tofauti na taarifa zilizoripotiwa.
EmoticonEmoticon