Bosi wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amekipa tano kikosi chake licha ya kupoteza mchezo dhidi ya wenyeji Weder Bremen ambao walimaliza mchezo wakiwa mbele kwa ushindi wa mabao matatu kwa moja.
Mourinho, amesema pamoja na kupoteza mchezo huo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi, yapo mengi mazuri aliyoyaona kutoka kwa wachezaji wake na pia ameahidi kuyafanyia kazi yalio machache ambayo yalisababisha kuangushiwa kisago cha mabao matatu.
Mourinho pia amekiri kufurahishwa na uwezo mkubwa ambao ulionyesha na mshambuliaji kutoka nyumbani Afrika katika nchi ya Ivory Coast, Tébily Didier Yves Drogba ambaye amerejea klabuni hapo baada ya kuondoka mwaka 2012.
Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini ureno ameahidi kuendelea kuitumia michezo ya kirafiki iliyosalia kwa ajili ya kukisua barabara kikosi chake kabla hakijaanza mshike mshike wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambao utaanza August 16 mwaka huu.
|
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon