TAARIFA RASMI YA BOMU LILILOONEKANA MTWARA




bomu
Hili ni bomu ambalo jioni ya June 16 2014 kwenye kijiji cha Mdui kata ya Mawala wilaya ya Mtwara vijijini kwenye mkoa wa mtwara liliokotwa na watoto waliokua wakicheza karibu na eneo la makaburi.Taarifa ilitolewa Polisi baadae ambapo baada ya wataalamu kuja na kuchunguza waligundua ni bomu la kurusha kwa mkono ambalo lina namba TNT MORTAR BOMB 60MM,LOT SOL 618 ambapo Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi walichukua hatua za kiusalama na kwenda kulilipua porini.

bomu4
Kaimu kamanda wa Polisi Mtwara Maisha Maganga ameongea na na kusema ‘ukiliangalia ni bomu ambalo ni la muda mrefu nadhani ni kipindi kile cha vita ya Msumbiji, tulilipeleka porini likalipuliwa na ulipuaji wake haukuwa na madhara… na sio kwamba ni bomu tunaweza kusema limeletwa ama imekuaje, ni bomu la muda mrefu tu’

bomu3
bomu2
Previous
Next Post »