TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 05.08.2014.
·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA
TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA UBAKAJI.
·
MTU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI AKUTWA
AMEUAWA NA MWILI WAKE KUTELEKEZWA BARABARANI.
·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUKATWA MAPANGA NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA WILAYANI MOMBA.
·
WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA WAKIWA NA MISIKOTO 13 YA BHANGI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA PETER TOSHI,
UMRI KATI YA MIAKA 25 – 30 ALIUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI.
TUKIO HILI
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 04.08.2014
MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA HUKO
MABATINI, KATA YA MABATINI, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA
TUKIO HILO INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA NA TABIA YA KUWAINGILIA KIMWILI
WANAWAKE BILA RIDHAA YAO WAKATI WANATOKA KUNYWA POMBE NA NDIPO HALI
ILIYOPELEKEA WANANCHI KUMSHAMBULIA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.
HAKUNA MTU
ALIYEKAMATWA KUHUSIKA NA TUKIO HILI. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO
HILI ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKATA KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA
HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA
ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 22 – 25
ALIKUTWA AMEUAWA NA MWILI WAKE KUTUPWA BARABARANI HUKU MIKONO YAKE IKIWA
IMEFUNGWA KAMBA KWA NYUMA NA PEMBENI YAKE KUKIWA NA MAWE PAMOJA NA FIMBO.
TUKIO HILI
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 04.08.2014
MAJIRA YA SAA 07:00 ASUBUHI HUKO
FOREST YA ZAMANI, KATA YA FOREST, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA TUKIO BADO HAKIJAFAHAMIKA. AIDHA TAARIFA ZA AWALI INADAIWA KUWA
MAREHEMU ALIUWAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
KWA TUHUMA ZA WIZI.
HAKUNA MTU
ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI
ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKATA KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA
HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JULIUS MARTIN
(54) MKAZI WA KITONGOJI CHA KALOLENI
ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE, TUMBONI,
MGONGONI, SHINGONI, BEGANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE
KUTUPWA/KUTELEKEZWA SHAMBANI.
TUKIO HILI
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 04.08.2014
MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA IVUNA, KIJIJI CHA IVUNA, KATA NA TARAFA YA KAMSAMBA,
WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILI BADO HAKIJAFAHAMIKA, JAPO
TAARIFA ZA AWALI INADAIWA NI KULIPA KISASI KWANI HAKUNA MALI ILIYOCHUKULIWA
IKIWEMO SIMU YA MKONONI. HAKUNA MTU ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILI,
JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU
UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SHIGELA MPENDARAIS (46) MKAZI WA
IKOJE – IVUNA NA 2. MAYUNGA MAONO (39)
MKAZI WA IKOJE – IVUNA WAKIWA NA MISOKOTO 13 YA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAMU 65.
WATUHUMIWA HAO
WALIKAMATWA MAJIRA YA SAA 02:00 USIKU
WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KALOLENI, KIJIJI CHA IVUNA, KATA YA
IVUNA, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA MSAKO
ULIOFANYIKA.
WATUHUMIWA HAO
WALIKUTWA NA BHANHI HIYO AMBAYO WALIIFICHA KATIKA MIFUKO YA PLASTIK NA KUIWEKA
KWENYE MIFUKO YA SURUALI. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA MBEYA BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA
YA MTUMIAJI.
Imetolewa na
[BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon